humph the GREAT
IMEFAHAMIKA kuwa mshambuliaji wa
Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu amesaini Klabu ya Long Tam Long An
inayoshiriki Ligi Kuu ya Vietnam.
Awali, mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Yanga, alikuwa akiwindwa na Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Timu hiyo ya Vietnam alikuwa akiichezea
Mtanzania, Danny Mrwanda kabla ya kurejea nchini na kujiunga na Yanga na
baadaye Majimaji ya Songea.
Kwa mujibu wa taarifa lilizozipata Championi Jumamosi, Kavumbagu anajiunga na timu hiyo kama mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
“Kavumbagu amesaini mkataba wa kuichezea
Klabu ya Long Tam Long An inayoshiriki Ligi Kuu ya Vietnam, hiyo ni
baada ya kufikia makubaliano na klabu hiyo.
“Awali, kabla ya mshambuliaji huyo
kusaini mkataba huo, alikuwa akitakiwa na Mbeya City ambayo ilishindwana
naye kutokana na kuhitaji dau kubwa la shilingi milioni 40,” alisema
mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad
Kawemba kuzungumzia usajili wa mshambuliaji huyo, alisema wao hawana
taarifa za mshambuliaji huyo kusajiliwa huko, wao wanachofahamu mchezaji
huyo mkataba wake ulimalizika msimu huu wa ligi kuu.
“Na kingine wachezaji wote ambao
mikataba yao imemalizika na wengine wote hatma yao itaamuliwa mara kocha
wetu atakaporejea nchini Julai Mosi, mwaka huu na timu kuingia
kambini,” alisema Kawemba.
Tags
Michezo na burudani