humph the GREAT
Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’
Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’
Stori: Humphrey \, blogger
DAR ES SALAAM: Mkali wa Hip Hop
Bongo, Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa anaheshimu
maneno ya msanii mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kuwa anamkubali na
kutamani kuwa na mwanaume mwenye sifa kama zake lakini yeye ana mpenzi
wake wa muda mrefu.
Estalina Sanga ‘Linah’
Akizungumza na Wikienda alipotembelea
Global TV Online wikiendi iliyopita, Darasa alisema kuwa Linah ametumia
ujasiri kutoa hisia zake na amefurahi kusikia anamkubali ingawa yeye
ana mpenzi wake wa muda mrefu na wanaaminiana.
“Namshukuru kwa kunikubali, kiukweli namheshimu na nimefurahi,” alisema Darasa.
Darasa alifunguka hayo baada ya hivi
karibuni Linah kueleza hisia zake kwenye mitandao ya kijamii kuwa
anatamani awe na mwanaume mwenye sifa alizonazo Darasa.
Tags
Udaku