humph the GREAT
MSANII wa Hip Hop mwenye ‘title’
kubwa Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amesema kuwa wasanii
wanaofanya gemu la Muziki wa Hip Hop nchini hawana budi kuiga ‘system’
ya jinsi anavyofanya kazi ili kuweza kufikia malengo yao hata kuwa
wasanii wakubwa, wenye heshima na mtaji wa mashabi lukuki.
Akichonga na Uwazi Showbiz,
Nay anayetamba na ngoma ya Saka Hela kwa sasa alisema watu
wanaomfuatilia wataona kuwa amekuwa na utaratibu mzuri hasa wa kutoa
kazi kwa kuangalia soko linataka nini na yeye afanye nini jambo ambalo
linamfanya awe juu kipindi chote.
“Unajua wasanii wengi wanashindwa
kufikia malengo yao kwa sababu hawafahamu namna ya kucheza na mashabiki,
mimi ninawataka wanifuatilie na kuiga mfano wangu waone kama
hawatafanikiwa kufika wanapotaka,” alisema Nay.
Tags
Burudani