humph the GREAT
BAADA ya kimya cha muda mrefu
msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, aliyewahi kutamba akiwa ndani ya Kundi
la Wanaume Familiy, Cheka Haji ‘Bi cheka’ ameibuka upya kwenye tasnia
hiyo baada ya kutoa ngoma kali inayokwenda kwa jina la Mapenzi ya Kale
Siku Hizi Hakunaga aliyomshirikisha mkali kwenye gemu la Muziki wa
Singeli, Marick Thadei ‘DJ Mack’.
Akichonga na Uwazi Showbiz,
kwa niaba ya Bi Cheka, DJ Mack amesema wimbo huo umepikwa na prodyuza
kutoka Natal Records aitwaye G Max na anaamini utafanya vizuri hata
kumrudishia Bi Cheka mashabiki waliokuwa wanamfuatilia.
“Wimbo ni mzuri kiukweli, ninatumaini
utafanya vizuri na kumrudisha Bi Cheka kwenye reli maana ni kimya sasa
kimepita tangu asikike kutokana na matatizo ya hapa na pale yanayoweza
kumpata binadamu yeyote,” alisema DJ Mack.
Tags
Burudani