JINA: PENZI LA SHEMEJI SNURA
MTUNZI: HUMBPHREY ENO MTWEVE
NAMBA: 0786549966
Ilipoishia
"we tatu!" baba alimuita mfanyakazi wetu wa ndani
"bee" ilisikika sauti ya tatu ikitokea ndani
"njoo mara moja"
"abee baba" aliitika tatu baada ya kumkaribia baba
Endelea nayo
"Sasa fanyeni hivi, sisi leo kwenye chakula cha mchana msituhesabie kwani uwezo wa kuwa hapa nyakati za mchana ni mdogo sana tunaweza tukala hukohuko, wewe cha msingi utapika chakula cha kula wewe na huyo mwenzako" alizungumza baba huku akiingia kwenye gari
"Okuy, tatu baadae" mimi na grace tulimwaga tatu
Na baada ya hapo wote watatu yaani mimi, baba na grace tuliingia kwenye gari na kuanza safari tulipokuwa ndani ya gari maongezi yaliendelea
"Daaah, eenhe niambieni leo tunaelekea wapi kwanza ?" baba alituuliza sisi
"aaah hata sijui wewe ndio wajua" nilimjibu huku grace na yeye akinisapoti kwa kichwa akiashili anakubaliana na mimi
"kwa hiyo ninyi hamjui tunakoenda ? nikiwapeleka chinja chinja je ?"
"hahahah.. baba na ulivyo muoga hivyo utaweza kumshuhudia mtu akichinjwa ?" nilimuuliza huku nikicheka sana
"haaaa! kwani wewe hujasikiaga kwamba mtu anamtoa kafara mwanae?"
"sawa lakini kuna watu am,bao ni wakatili hivyo na kulifanya hilo wanaona kwao ni kazi rahisi tuu lakini sio wewe, yaani wewe hata siku moja sijawahi kukuona hata ukitufokea tuu zaid zaid mama ndo alikuwa kidogo tunamuelewa kwa viboko vyake"
"hahah haya buana, niachieni mimi basi leo nikawalishe "
"na mimi siku moja nitawatoa out kama hivi" alisema grace
"hahahha ndo ukomae" tuklimjibu mimi na baba huku tukicheka sana
"nyie chekeni tuu ila ukweli ndio huo" alisema grace
Basi stori nyingi ndizo zilitufanya tuione safari kama ni fupi hivi, na hatimaye tulifika mjini ni mwendo wa kama lisaa limoja hivi mpaka kufika mjini, na baada ya kufika mjini ndipo tukaingia hotelini na baba kututaka sisi tuanze kuagiza chakula
"mie naomba chips kuku" aliongea grace
"mie nipe soseji mbili na kuku rost" niliagiza mimi wakati huo baba alikuwa ametoka nje kidogo, baada ya kurudi na yeye aliagiza
"hahah! ndio maana vijana wa siku hizi m,nakuwa legelege"
"vipi kwani mZee?" nilimuuliza nikimuangalia mzee
"wewe mtoto wa kiume utaagizaje soseji"
"hahah baba na wewe kwa hyo tulitakiwa kula nini?"
"ngoja subir mimi niagize chakula ambacho mwanaume unatakiwa kula" aliongea baba
"we mhudumu nipe chapati nne na maziwa freshi" baba aliagiza baada ya mhudumu kupita karibu yake
"haaa! we baba" nilimuita kwa mshangao
"chapati ngapi?"
"kwani hujaskia nnavyoagiza au, et mwanangu grace wewe si umesikia nilivyo agiza ee?"
"ndio baba nimesikia " alijibu grace akiwa anacheka
"haya mwambie mwenzako manake inaelewezekana siku hizi kaka yako masikio hayafanyi kazi vizuri"
"Si umesema chapati nne na maziwa fresh kikombe kimoja"
"haya umesikia?" baba aliniuliza huku akiniangalia mimi usoni huku akiwa na tabasamu
"sio kwambasikusikia "
"ila?" baba alihoji huku akipokea chakula chake kutoka kwa mhudumu
"wewe utamaliza chapati zote hizo?"
"sasa kwanini nisimalize vichapati vyenyewe vidogo vidogo hivi"
"mmmm" niliguna
"haya wanangu enjoy your food"
Baada ya hapo wote tuliendelea kupata chakula huku stori za hapa na pale zikiendelea kwani tulikuwa watu tusioishiwa na stori, na baada ya kula baba akatuuliza tungependa kwenda wapi? kwa wakati ule wote tukasema kwa sababu leo ni siku tusiyokuwa na kazi na wewe baba ameamua kututoa out basi tukamwambia tunataka kwenda suprise beachh ambayo ipo maeneo ya makambako
"haaa! nyie watoto?"
"vipi baba?" nilimuuliza nikimtazama kwa makini wakati tunatoka hotelini baada ya kupata chakula
"mbona huko mimi mwenyewe sikufahamu, halafu ni mbali hivyo?"
"sasa baba sehemu ambayo hujawahi kufika si ndo vizuri kwenda kutoa ushamba jaman" aliuliza grace akimuangalia baba wakatio anafungua mlango wa gar
"Haya twendeni mtakuwa mnanielekeza "
"wewe si ndo dereva hivyo inakupasa uwe unasoma alama za barabarani na bango lenyewe utaliona" nilimwambia kiutani
"mambo haya ndio maana mimi nikasema ray aendeshe gari"
"hahah, mambo yenyewe haya ndio maana nilisema sitaki kushika uskani leo"
bas tulitoka maeneo ya mafika mida kama saa nne hivi kuelekea makambako ambako mimi na grace tulidai tunataka kwenda kwa siku hiyo kwani ni mara yetu ya kwanza kwenda huko, ilichukua kama masaa mawili na kidogo mpaka kufika huko kwani hatukupata shida hata kidogo na baada ya baba kumuonrsha kibao ambacho kinaelekeza hiyo sehemu ilipo kabla hatujafika makambako mjini... na baba akakunja tukaelekea mpaka kwenye geti la kuingilia na tukaelekezwa utaratibu na tukaenda pia mapokezi baba akafanya malipo yote kwa muda wote tutakao kuwa mle ndani tulikaa muda mrefu kweli na pia tukapata chakula cha mchana na baada ya kupata chakula cha mchana ndipo tukaanza safari ya kurudi mafinga kwa kuwa tulikuwa tumechoka sana wakati wa kurudi tulikuwa hatuna muda wa kupiga stori tena ndani ya gari hivyo kutufanya tufike upesi mafinga ni baada ya muda wa kama masaa mawili hivi tukawa tayari tumeshafika mafinga lakini nilimuomba baba niwapeleke home theni mimi nirudi kwani nilipanga kwenda iringa kumuona girlfriend wangu.
"Sasa baba"
"ndio mwanangu"
"mi nina safafri ya kwenda iringa nilikuwa nina shida kidogo kule "
"kwa hiyo ulikuwa unasemaje?"
"nilikuwa nataka nikuage na kama utaweza kunipa hela kidogo ya matumizi"
"kwa hiyo utaenda na gari gani?"
"yoyote ile?"
"au hii hii?"
"aaah baba tangu lini umeniona mimi naendesha gari hii?"
"mm vip mwenzako mbona haongei amelala nini?"
"hee! amelala tokea muda sana mbona"
"aahaa ok ngoja tufike nyumbani basi, tutalizungumzia hilo"
"ok ok"
Baada ya kama dakika 40 hivi ndipo tukawa tunaingia nyumbani ikiwa imetimu mida ya kama saa kumi na moja jioni, na baada ya baba kumueleza akaniambia ninahitaji kiasi gani cha pesa nikamwambia chochote akanipa laki 2 lakini pia akaniambia hela nyingine atarushia kwenye account yangu ya bank kwani hako nazo mfukoni kwa wakati ule, nilimuuliza kama gari zina mafuta akadai ambayo itakuwa haina mafuta ni hii ambayop tumefika nayo kwa sasa
"duh wewe mutru huwa huchoki safari au?" aliniuliza grace
"kwani vipi"
"sasa wewe tumetoka kufika sasa hivi na penyewe safari ilivyokuwa ndefu vile lakini bado kumbe mwenzetu
uko na mipango ya safari nyingine" aliongea grace akikaa kwenye moja ya sofa lililokuwa pale sebuleni
uko na mipango ya safari nyingine" aliongea grace akikaa kwenye moja ya sofa lililokuwa pale sebuleni
"hahah yani wewe hii safari yenyewe ya kusimama mara mnashuka mnapumzika mnakula na kula halafu unasema eti ni safari ndefu wewe hujasafiri safari ndefu wewe, mimi hapa uchovu ndo hata kidogo hivi baba akisema twende shamba apa naliamsha"
"mwanangu twebde bustanini apo" aliongea baba huku akitoka kutoka ndani ambnako alikwenda kuabadilisha nguo akiwa amevaa mabuti ya shamba
"nenda sasa" aliniambia grace akiwa anacheka sana
"sasa baba mi napanga safari wewe unaniambia twende shamba tena?"
"hahaha nilikuwa nakutania tuu, endelea na mipango yako buana"
"nyooo, mbona unajitetea ungeenda na baba" alisema grace
"ningeenda isingekuwepo safari hii"
"wewe afande!" nilimuita mlinzi wa pale getini
"naam bosi"
"toa ile gari pale ile nyeusi ile" niliongea na kumkabidhi funguo
"aaha sawa bos" alinijibu huku akiondoka
"hivi ray ile gari mbona unaipendaga sana kwanini" aliniuliza grace
"ile ndo gari ya kisasa na yenye swaggz"
"mmmm haya buana, haya hebu niambie unaenda kufanya nini huko iringa?"
"kuna jamaa nilimuagiza mzigo fulani hivi so amesema niende nikaucheki, manake imekuja mingi kwenye oda yake"
"aaahaa poa poa safari njema"
"bos tayari lipo nje"
"funguo ziko wapi?"
"nimeziacha ndani ya gari"
"haaa!! ila wewe sasa wakibeba kule"
"si unaondoka sasa hivi bosi"
"mmh grace ee ngoja mi niende bwana, utaniagia kwa mzee na tatu" niliondoka na kutoka nje
kwa kuwa nilikuwa peke yangu hivyo sikuwa na mtu wa kupiga naye stori zaidi ya kufungulia muziki ndani ya gari na kukanyaga mafuta nilienda kwa spidi kidogo mpaka mida ya saa kumi na mbili na madakika yake nikawa nimeingia iringa mjini na kuchukua chumba moja ya rodge moja pale town, baada ya kuoga na kupumzika vya kutosha nikaamua kuwasiliana na mchumba wangu mmoja hivi ambaye alikuwa anasoma RUCU na kumuuliza kama inawezekana akaja mpaka nilipo mimi kwani safari ya kutoka mafinga ilikuwa ni ya kumfuata yeye tuu hakuna lingine kwani mzigo ulikuwa sio wa muhimu sana na ulikuwa ni viatu na simu mbili ambazi nilimuagiza jamaa yangu mmoja ambaye ni mfanya biashara ambaye yupo hapa mjinoi
Baada ya kuongea na merry akaniambia uwezekano huo upo lakini itabidi niende kumchukua kwani alikuwa bado yupo kwenye discussion na wenzake ambao wapo naye group moja. Na aliponipigia simu kwamba yuko tayari nilifunga safari mpaka chuoni na baada ya kufika getini nilijieleza mpaka nikaruhusiwa na kuingia ndani.
itaendelea....
0 Comments