Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
WACHAMBUZI wa masuala ya soka katika runinga ya Al Ahly, wametumia takribani dakika kumi wakiichambua penalti ya kwanza ya Yanga iliyopigwa na nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Zaidi wachambuzi hao walikuwa wakitumia neno halua, kuonyesha ni kitu kizuri na namna ambavyo kipa wa kikosi chao alivyoteseka.
Cannavaro ndiye alikuwa wa kwanza kupiga penalti kwa upande wa Yanga katika mechi dhidi ya Al Ahly iliyopigwa Jumapili iliyopita jijini Alexandria na Yanga kung’olewa kwa penalti 4-3.
Hata katika mitaa ya Cairo, mashabiki wa soka kila wanapowaona wachezaji wa Yanga au Watanzania wamekuwa wakiizungumzia penalti hiyo, wakitumia neno halua, yaani safi au nzuri.
Yanga inaondoka jijini hapa leo usiku kwa ndege ya Shirika la Ndege la Egypt na inatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam saa 12, asubuhi.
Tags
Michezo na burudani