REAL MADRID YAIPIGA 5-0 BAYERN, YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA






Shangwe: Wachezaji wa Real Madrid wakiwa na shangwe za kutinga fainali.

Kamba: Sergio Ramos akiifungia Real Madrid bao la kwanza dakika ya 16.

Chenga la mwili: Mshambuliaji hatari wa Bayern Munich, Franck Ribery (kushoto) akimtoka Gareth Bale.

Ndoo: Sergio Ramos akicheka na nyavu kwa mara ya pili katika dakika ya 20.

Mwanaume kazini: Cristiano Ronaldo akiifungia Madrid bao la tatu dakika ya 34.

Yametimia: Cristiano Ronaldo akishangilia na Gareth Bale baada ya kufunga bao la nne dakika ya 89.

Hoi: Wachezaji wa Bayern Munich wakiwa hawaamini kilichotokea nyumbani kwao.
TIMU ya Real Madrid imetinga fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kuitandika  Bayern Munich mabao 4-0 katika Nusu Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani usiku huu.
Bayern wamevuliwa ubingwa wa Ulaya kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-0, baada ya awali kuchapwa 1-0 Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid katika Nusu Fainali ya kwanza na Real inaingia Fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, ambako itakutana na ama Chelsea au majirani zao Atletico Madrid ya Hispania pia.
Shujaa wa Real alikuwa ni Sergio Ramos aliyefunga mabao mawili, la kwanza dakika ya 16 pasi ya Luka Modric na la pili dakika ya 20 pasi ya Pepe kabla ya Mwanasoka wa Bora Dunia, Cristiano Ronaldo kumaliza kazi kwa kufunga mabao mawili dakika ya 34 pasi ya Gareth Bale na dakika ya 89.
Bayern Munich: Neuer, Lahm, Dante, Boateng, Alaba, Schweinsteiger, Kroos, Ribery/Gotze dk73, Muller/Pizarro dk73 na Robben, Mandzukic/Martinez dk46.
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane dk75, Coentrao, Alonso, Modric, Di Maria/Casemiro dk84, Ronaldo, Bale na Benzema/Isco dk80.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post