ILIPOISHIA WIKIENDA
Sikupata jibu. Tukio hilo nililiona kama kitisho kikubwa ambacho nisingeweza kukiepuka.
Laiti kama Nikole angenifia gesti ningeweza kumuacha na kumkimbia. Lakini amefia nyumbani kwangu mahali ambapo nisingeweza kumkimbia.

Kwa sababu ya kuchanganyikiwa nilitoka nje, nikaketi barazani. Nilidhani nikikaa hapo nje ningeweza kuwaza kwa busara na kupata ufumbuzi wa tatizo lililokuwa limenikabili. SASA ENDELEA…
Macho yangu yalikuwa kwenye nyumba za majirani na kwa watu waliokuwa wanapita barabarani. Isingekuwa rahisi kwa majirani kujua kilichotokea nyumbani kwangu. Kilichotokea bado ilikuwa ni siri yangu lakini sikujua siri ile ingedumu kwa muda gani.
Pale barazani pia sikukaa kwa muda mrefu, nikarudi ndani. Kusema kweli nilikuwa natangatanga tu bila kujua nifanye nini kwani kila hatua niliyopanga kuchukua ilikuwa ngumu. Kifo kama kile cha Nikole kilipaswa kuripotiwa polisi. Lakini nikienda kuripoti polisi, mimi mwenyewe ndiye nitakayekuwa mtuhumiwa namba moja. Nitakamatwa hapohapo na kuwekwa ndani. Na kwa kesi hizi za mauaji ambazo hazina dhamana, nikiwekwa ndani ndiyo nimeshapotea! Kwa sababu hiyo wazo la kwenda polisi sikuafikiana nalo.
Lilinijia pia wazo la kuupeleka mwili wa Nikole hospitali. Lakini nilijua ni lazima madaktari watataka nikatoe ripoti polisi. Wazo hilo nalo niliona halifai.
Siku ile ikapita bila ya mimi kufanya kazi. Kila wakati nilikuwa naenda kule stoo kuichungulia maiti ya Nikole kama vile nilitarajia nitamkuta Nikole mwenyewe akiwa hai. Usiku ulipowadia niliingia chumbani kwangu mapema, nikajilaza kitandani. Wakati naendelea kuwaza simu yangu ikaita. Niliposikia mlio wake nilishituka.
Nikaitazama kisha nikaichukua. Niliona namba iliyokuwa inaita ilikuwa ngeni kwangu.
Nikajiuliza ni nani anayenipigia huku nikijaribu kuitafakari ile namba. Sikuweza kukumbuka ilikuwa namba ya nani, nikaamua kuipokea simu.
Nikajiuliza ni nani anayenipigia huku nikijaribu kuitafakari ile namba. Sikuweza kukumbuka ilikuwa namba ya nani, nikaamua kuipokea simu.
“Hallo!”
“Habari ya saa hizi?” Ilikuwa sauti ya kike iliyotokea katika simu ya upande wa pili.
“Nzuri, nani mwenzangu?”
“Ni mimi Asma.”
“Habari ya saa hizi?” Ilikuwa sauti ya kike iliyotokea katika simu ya upande wa pili.
“Nzuri, nani mwenzangu?”
“Ni mimi Asma.”
“Asma…Asma yupi?” nikamuuliza huku nikijaribu kumtafakari huyo Asma akilini mwangu.
“Ina maana umenisahau. Mbona mimi bado nakukumbuka.”
“Hebu nikumbushe tulikutana wapi?”
“Hapahapa Ilala. Kwani uko wapi muda huu?”
“Niko nyumbani.”
“Ina maana umenisahau. Mbona mimi bado nakukumbuka.”
“Hebu nikumbushe tulikutana wapi?”
“Hapahapa Ilala. Kwani uko wapi muda huu?”
“Niko nyumbani.”
“Unaweza kufika hapa Maua Hotel. Nina mazungumzo na wewe.”
“Kuhusu nini?”
“Kuhusu Nikole.”
“Kuhusu nini?”
“Kuhusu Nikole.”
Moyo ukanipasuka paa!
“Nikole ni nani?” nikajidai kumuuliza.
“Mke wa Machibya.”
Inaelekea huyu msichana anafahamu mengi kuhusu mimi, nikajiambia.
“Machibya namfahamu.” nikamwambia.
“Nikole ni nani?” nikajidai kumuuliza.
“Mke wa Machibya.”
Inaelekea huyu msichana anafahamu mengi kuhusu mimi, nikajiambia.
“Machibya namfahamu.” nikamwambia.
“Hukumbuki kwamba mimi ndiye niliyemleta kwako kwa mara ya kwanza ili umtafutie nyumba?”
Hapo hapo nikamkumbuka niliyekuwa nazungumza naye.
“Nimekukumbuka Asma wa Ilala, nilikusahau kidogo.”
Hapo hapo nikamkumbuka niliyekuwa nazungumza naye.
“Nimekukumbuka Asma wa Ilala, nilikusahau kidogo.”
Alikuwa msichana ambaye nilikuwa nafahamiana naye pale Ilala. Watu walikuwa wakimuita Asma wa Ilala. Aliwahi kuniletea wateja akiwemo Machibya ili niwatafutie nyumba.
Sasa nikawa nimepata jibu kwa nini alimfahamu Nikole. Lakini sikupata jibu alikuwa na mazungumzo gani na mimi kuhusu Nikole.
Sasa nikawa nimepata jibu kwa nini alimfahamu Nikole. Lakini sikupata jibu alikuwa na mazungumzo gani na mimi kuhusu Nikole.
“Sasa mazungumzo ya mke wa Machibya yananihusuje mimi?” nikamuuliza.
“Yanakuhusu sana,” akaniambia na kuuweka moyo wangu juu!
“Yananihusu kivipi?”
“Yanakuhusu sana,” akaniambia na kuuweka moyo wangu juu!
“Yananihusu kivipi?”
“Ndiyo maana nikakuita uje hapa tuzungumze.”
“Lakini ni mazungumzo mazuri?”
“Utakuja kuyasikia.”
“Lakini ni mazungumzo mazuri?”
“Utakuja kuyasikia.”
Nikaguna kabla ya kumuuliza; “Umesema uko hapo Maua Hotel?”
“Ndiyo, njoo. Nakusubiri.”
“Nakuja.”
“Usichelewe.”
“Nakuja sasa hivi.”
“Sawa.”
“Ndiyo, njoo. Nakusubiri.”
“Nakuja.”
“Usichelewe.”
“Nakuja sasa hivi.”
“Sawa.”
Nikashuka kitandani na kuvaa nguo haraka haraka. Moyo wangu ulikuwa umeshapatwa na wasiwasi mwingine. Sikujua huyo msichana alitaka kunieleza nini kuhusu Nikole. Baada ya kuvaa nilitoka. Hoteli ya Maua ambayo ilikuwa maarufu pale Ilala ilikuwa mtaa wa pili baada ya ule niliokuwa ninaishi mimi. Sikuhitaji usafiri. Nilifika kwa miguu muda uleule tu.
Nilimkuta Asma akinisubiri nje ya lango la kuingilia kwenye hoteli hiyo. Alikuwa amesimama kando ya lango hilo.
“Ndiye wewe Asma au macho yangu?” nikamuuliza.
“Ndiye mimi. Nilikuwa ndiyo natoka.”
“Ulikuwa unasemaje?” nikambandika swali hilo haraka.
“Nikole yuko wapi?” akaniuliza.
Swali lake lilinishitua sana.
“Ndiye wewe Asma au macho yangu?” nikamuuliza.
“Ndiye mimi. Nilikuwa ndiyo natoka.”
“Ulikuwa unasemaje?” nikambandika swali hilo haraka.
“Nikole yuko wapi?” akaniuliza.
Swali lake lilinishitua sana.
“Mbona unaniuliza mimi, nitajuaje aliko?”
Asma akacheka.
Asma akacheka.
“Nimekuuliza hivyo kwa sababu najua ni mpenzi wako”
“Hapana. Nikole si mpenzi wangu na sina uhusiano naye.”
“Mume wake alisafiri jana kwenda Tabora. Nikole aliniambia atakuja kwako lakini sijamuona hadi leo.”
Je, nini kiliendelea? Usikose kufuatilia simulizi hii ya kusisimua kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda siku ya Jumatatu.

“Aje kwangu kufuata nini?”
“Anajua mwenyewe lakini mimi aliniambia anakupenda sana. Unajua tangu siku ile nilipowaleta kwako uwatafutie nyumba Nikole amekuwa rafiki yangu sana. Siri zake zote ananieleza. Kuna jambo moja la hatari amelifanya…”

Tags
Hadithi & Simulizi