Chungu cha ajabu kilichokutwa juu ya kaburi la mtoto Agnes Mlawa katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa leo kikiwa kinafoka damu.
Baada ya kufunguliwa chungu hicho ndani kulikuwa na damu, maini na kichwa cha ndege.
Wananchi wakishuhudia chungu hicho cha ajabu kilichopo kushoto karibu na jembe.
Baba wa mtoto Agnes Mlawa akichimbua chungu hicho.
Baba wa mtoto huyo kulia akisaidiwa na msamalia mwema kufungua chungu hicho.
Msamaria mwema akionyesha vitu vilivyopo ndani.
Mzee Mlawa akiwasha kiberiti kwa ajili ya kuteketeza chungu hicho.
Chungu kikiteketezwa kwa moto.
Wananchi na mzee Mlawa (kulia) wakitazama tukio la kuteketezwa chungu hicho.
MAUZAUZA yametokea katika kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana baada ya baba wa mtoto huyo kukuta chungu cha ajabu chenye damu, maini na kichwa cha ndege kaburini hapo.
Tukio hilo la aina yake limetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa wakati baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa akichembua kaburi hilo na mara baada ya kumaliza ghafla alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo.
"Mimi nilikuja hapa kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka juu kutoka kaburini na baada ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka juu ya kaburi "
Alisema kuwa chungu hicho kilikuwa kimefunikwa na kitambaa cheusi juu ambacho kililowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na tukio hilo la ajabu alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita watu wanaopita barabarani ili kuomba msaada.
Mzazi huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki dunia.
Hata hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake haamini mambo ya kishirikiana hakuona sababu ya kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia zoezi la kuchoma chungu hicho na badala yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe hasa akiamini katika nguvu ya Mungu.
"Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia nguvu na pia kuwashukuru madereva bodaboda akiwemo kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta ya petroli kwa ajili ya kukichoma chungu hiki "
Mbali ya mzazi huyo kujitolea kuchoma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyokuwemo ndani, wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo walilazimika kutimua mbio wakihofia zoezi hilo la uchomaji wa chugu.
Tags
maajabu