MWIGIZAJI ambaye ambaye alikuwa akifanya kazi kwa karibu sana na marehemu Steven Kanumba, Mayasa Mrisho ‘Maya’ alijikuta akishindwa kuhudhuria siku maalum ya marehemu baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa malaria.
Mwigizaji wa Bongo Muvi, Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Siku ya Kanumba Day iliadhimishwa Jumatatu iliyopita ambapo ndugu pamoja na baadhi ya wasanii walijumuika pamoja kufanya maombi kanisani, kwenda makaburini kumkumbuka marehemu kisha sherehe katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem, jijini Dar, lakini Maya alishindwa kutokana na kuumwa huko.
“Nilizidiwa ghafla siku ya Jumapili, nikalazwa katika dispensari ndogo hapa nyumbani Magomeni lakini baada ya kuanza dozi siku ile, naendeleda vizuri, wameshaniruhusu,” alisema Maya.