MTOTO WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, RIDHIWANI KIKWETE AMEELEZA NIA NA NDOTO YAKE YA KUWA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) SIKU ZA USONI.
Ridhiwani Kikwete ameeleza ndoto yake hiyo katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm, wakati akijibu swali kuhusu nafasi ya uongozi anayoipenda zaidi, swali lililoulizwa na Fred ‘Fredwaa’ Fedilis.
“Mimi wishes zangu…wishes zangu mimi ni siku moja kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ndio mwisho.” Amesema Ridhiwani Kikwete.
Ameeleza jinsi makatibu wakuu wa Chama cha Mapinduzi walivyofanya kazi nzuri, na kukoa mfano wa kazi inayofanywa na Abdulrahman Kinana kuwa ni kazi ambazo alikuwa anatarajia kuzifanya.
“Comrade Kinana anafanya kazi ambayo mimi binafsi nilikuwa nawish niifanye, umenielewa. Kwa lugha nyingine ni kwamba naamini ili nchi itulie lazima chama kitulie. Na mimi naamini kwamba destination yangu ni kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi. Na siku moja ntakuwa tu.” Amefafanua Ridhiwani.
Ridhiwani Kikwete ambaye hivi sasa anagombea ubunge wa jimbo la Chalinze alieleza kuwa sio kwamba hautaki urais kama anavyouhitaji ukatibu mkuu kwa kuwa siku zote hupenda kuwa chini kidogo ili aweze kuwashauri walio juu yake.
“Si kwamba sihitaji nafasi ya urais, isipokuwa mimi siku zote sio mtu ambaye anatamani kuwa mkubwa. Kama umefuatilia historia ya maisha yangu siku zote nimekuwa nagombea nafasi za ushauri.” Ameeleza.
Ametaja nafasi mbalimbali alizowahi kushika katika chama ambazo sio nafasi za ngazi ya juu na kueleza sababu ya kupenda kuwa katika ngazi hizo.
“Kwa nini nagombeaga nafasi hizo…nagombea nafasi hizo kwa kuwa nina uwezo mkubwa sana wa kuona mwenzangu anakosea wapi. Nina uwezo mkubwa sana wa kuona nishauri nini ili mambo yakae vizuri. Kwa hiyo ndio maana naamini kwamba nitakapo katibu mkuu wa chama cha mapinduzi siku moja, ntakuwa na nafasi kubwa sana ya kumshauri mwenyekiti wangu juu ya jinsi gani tunaweza kuendesha chama na serikali. Kwa sababu chama chetu sisi unapokuwa mwenyekiti ndio unakuwa rais. Kwa hiyo naamini ni nafasi kubwa sana ya kushauri kuliko ya mimi kuwa mbele kutenda.”
Kipindi cha Sun Rise kinakuwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu kamili asubuhi.
http://www.hulkshare.com/timesfmradio/ridhiwani-kikwete-akiongea-na-sun-rise-ya-times-fm
Tags
Ccm