IKIWA imesalia wiki moja kabla ya kukutana uso kwa uso na Yanga, straika wa Simba, Amissi Tambwe ametamba kuwa lazima afunge bao katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe anayeongoza kwa mabao katika ligi hiyo akiwa amecheka na nyavu mara 19, alisema jeuri hiyo anaipata kwa sababu ukuta wa Yanga hauna mchezaji wa kumzuia.
Tambwe…

Tambwe ameendelea kujinadi kuwa Yanga ni timu ya kawaida na hata safu yake ya ulinzi ni nyepesi, ndiyo maana anatoa kauli kwa kujiamini.

“Nashukuru Mungu hivi sasa nipo vizuri, maumivu niliyokuwa nayo hapo awali hayapo tena, nguvu zangu zote naelekeza katika mechi zilizosalia, hasa ile dhidi ya Yanga.
“Naamini kuwa itakuwa ngumu lakini nitahakikisha nafunga ili niweze kujijengea heshima zaidi hapa nchini, katika kikosi cha Yanga hakuna beki wa kunizuia kufunga kwani wote ni wa kawaida kama walivyo wa timu nyingine,” alisema Tambwe huku akionyesha kujiamini.

Tags
Michezo na burudani