Kama Diamond Platnumz angekutana na Eiden usiku wa kuamkia Jumamosi ya leo, huenda angemfanya mwanamke huyo wa kizungu kuwa mwenye furaha kuliko watu wote duniani. Mwanamke huyo ambaye usiku huo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 32, anadai alisafiri kutoka nchini Rwanda kuja jijini Dar es Salaam ili amtafute hitmaker huyo wa ‘Number One’ amuimbie wimbo maalum wa siku ya kuzaliwa.
Bahati mbaya, mara tu baada ya kutumbuiza kwenye show ya Road to MAMA, aliwahi ndege ya kwenda jijini London, Uingereza kuwahi show yake na Ommy Dimpoz na kuizima ndoto ya Eiden.
“Mimi ni shabiki mkubwa zaidi wa Diamond duniani,” Eiden aliiambia Bongo5. “I want him to sing me happy birthday cause I am his number one fan and I’m not married I have no kids and I am not ashamed. I just love him and I think I feel like he needs to meet me, If he doesn’t meet me his life is not gonna be the same. I am incredible, if he doesn’t know me he is just gonna be a poor person in the world.”
0 Comments