Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeagiza vyombo vya dola, kukamata waganga wa jadi, wanaojitangaza kutibu magonjwa ya Ukimwi, kisukari na
shinikizo la damu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dk Seif Rashid alipokuwa akiwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya
Wizara yake
kwa
mwaka wa fedha 2014/15.
Aliwasihi wataalamu wa tiba asili na tiba mbadala, kuacha mara
moja,
kujitangaza kuwa
na uwezo wa kutoa tiba dhidi ya ugonjwa wowote ule ambao
uwezo huo haujathibitishwa
kitaalamu.
“Hilo ni kosa kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha tiba asili na tiba
mbadala,”
alisema.
Waziri huyo alisema yapo matangazo yanayohusu kuwa na uwezo wa
kutibu Ukimwi,
kisukari
na shinikizo la damu. “Kwa mujibu wa Sheria ya Tiba asili na Tiba mbadala, matangazo
hayo
yaondolewe mara moja,” alisema.
Alieleza kuwa wizara itatoa mwongozo na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili dawa husika
zithibitishwe kitaalamu.
“Napenda kuchukua fursa hii kuagiza vyombo husika vya serikali, vifuatilie kwa karibu na
kuchukua hatua kwa mujibu wa sheriakwa wale watakaokwenda kinyume na sheria,”
alisema.
Waziri huyo pia alizungumzia suala la tiba za kibingwa, ili
kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi kwa uchunguzi na
matibabu.
Alisema Wizara inaendelea kuanzisha huduma za tiba za kibingwa katika hospitali za Kanda,
hospitali Maalum na Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kupunguzwa wagonjwa hao wa kwenda
nje ya nchi.
Alisema huduma za upasuaji mkubwa wa moyo, zimeendelea kutolewa ambapo hadi
sasa wagonjwa 671 walipata huduma hiyo kwa mafanikio katika hospitali za Muhimbili,
Bungando na KCMC.
Aidha, wagonjwa 211 walifanyiwa upasuaji maalum katika
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), ambapo 29 walifanyiwa upasuaji wa ubongo,
107 upasuaji wa uti wa mgongo,
56 waliwekewa viungo bandia vya nyonga na 19 viungo bandia vya goti.
Dk Rashid alisema katika mwaka 2014/15 Taasisi ya Mifupa Muhimbili inatarajia
kuwahudumia wagonjwa wapatao 6,900.
Aidha, itafanya upasuaji wa kuweka viungo bandia vya nyonga kwa
wagonjwa 400,
kuweka viungo bandia vya goti kwa wagonjwa 150, upasuaji wa ubongo kwa
wagonjwa 240,
upasuaji wa uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kwa wagonjwa 400 na upasuaji wa
watoto
wenye vichwa vikubwa 600.
Bajeti aliyoomba ili kuiwezesha Wizara yake kutekelezwa kazi zilizopangwa katika
mwaka 2014/15, Waziri huyo aliomba Bunge kuidhinisha makadirio ya matumizi ya
wizara hiyo pamoja na taasisi zake yenye Sh bilioni 622.95, ambapo kati ya hizo
Sh bilioni 317.22 ni kwa ajili ya matumizi ya kwaida na Sh bilioni 305.72 ni
kwa ajili
ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Tags
mTAANI KWETU