humphrey the GREAT

Mtangazaji kutoka clouds fm millardayo
Mtangazaji kutoka clouds fm millardayo
MTANGAZAJI mwenye sauti nzito Bongo kupitia Clouds FM, Millard Ayo, Jumatatu iliyopita alibanwa azungumzie uhusiano wake na warembo wenye majina makubwa nchini, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo alimfungukia mmojammoja.
Katika mahojiano maalum na Kipindi cha Sporah Show, mtangazaji alimbana Millard akimtaka aseme ukweli kuhusu warembo hao ambapo alianza kwa kumzungumzia Lulu kuwa hajawahi kuwa mpenzi wake zaidi ya kumfahamu katika sanaa.
Jacqueline Wolper Massawe akiwa katika pozi.
Kuhusu Lulu! Hapana sijawahi kabisa kuwa na uhusiano naye. Yaani hata kuwaza sijawahi. Namfahamu kuwa ni mwigizaji na ni mtu ambaye nimekuwa nikimfuatilia kupitia kazi zangu za utangazaji,” alisema mtangazaji huyo staa.
Millard aliendelea kupangua, ikafika zamu ya Wolper. Alikana vikali kuwa naye hata kujuana kwao si kwa ukaribu. Alisema:
“Haa! Wolper ndiyo kabisa, nimekuwa nikimuona na kumsikia tu, wala sikuwahi kumuwazia kwa lolote lile isipokuwa ninamjua kama msanii wa Bongo Muvi na huwa nakutana naye kama ninavyoweza kukutana na mtu mwingine yeyote ambaye hatujuani.”
Millard akiwa na Jokate.