humphrey the GREAT
waziri wa habari, utamadyni na micchezo na sanaa
mh. nnape nauye katikati akiwa pamoja na maofisa wa jeshi
na wachezaji wa timu za soka, wakatim wa uzinduzi wa mashindano ya mkuu wa
majeshi, uwanja wa uhuru dar es salaam.
SERIKALI imesema inapenda kuona Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) linarudisha zama zake za kuibua wachezaji wenye uwezo wa kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa wachezaji maarufu wa enzi hizo akiwemo Filbert Bayi, Juma Ikaanga na Samson Ramadhan.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katika sherehe za ufunguzi wa muhula wa tatu wa mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Waziri Nape alisema changamoto iliyopo hivi sasa kwa timu za taifa ni kupata matokeo mabaya pindi zinaposhiriki kwenye mashindano ya kimataifa na hivyo, kushindwa kuleta ushindi na medali mbalimbali kama ilivyokuwa zamani.
“Sote tunafahamu kuwa miaka ya zamani timu za majeshi nchini ndizo zilizotoa uwakilishi bora katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, hivyo ni kiu ya wapenda michezo wengi mimi nikiwa mmojawapo kuona enzi hizo za jeshi kuwa kituo bora cha michezo na kuirudisha katika hadhi yake,” alisema.
Tags
Michezo na burudani