humph the GREAT
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda katika pozi
Mwanamuziki nchini Tanzania, Nuh
Mziwanda, ameamua kuvunja ukimya na kufuta tattoo yenye jina la
aliyekuwa mpenzi wake Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kabla ya kupata mbadala
wake.
Awali baada ya kutengana Nuh, alidai
kuwa tattoo ya Shishi, haimuumizi kichwa kwa kuwa aliichora kwa mapenzi
yote na sio kwa kuigiza hivyo kutengana kwao sio sababu ya kufuta tattoo
hiyo.
Nuh, ameshindwa kuonesha uvumilivu
kuiona tattoo hiyo na kudai kuwa baada ya kuachana na mrembo huyo
amekuja kujua kuwa Shishi, hakuwa mbadala wake sahihi kwani amekuwa
akimfanyia vituko mbalimbali.
Amedai kuwa mrembo huyo amekuwa akitumia
mtandao wa kijamii kumtukana pia kupitia mahojiano mbalimbali jambo
ambalo amekuja kujua hakuwa mtu mzuri wake
Sambamba na hilo Nuh, mbali na kuchora
tatoo mpya juu ya ile ya Shishi Baby, ameongeza tatoo nyingine kadhaa
mwilini kwake ikiwepo usoni.
Wawili hao wameachana siku za hivi
karibuni huku kila mmoja akificha chanzo cha penzi lao kuota mizizi na
hivyo kufikia hatua ya kila mtu kufuta tattoo ya jina la mpenzi wake.
Tags
wasanii