humph the GREAT
SHIRIKISHO la Soka Afrika (Caf),
limemruhusu beki mpya wa pembeni, Hassan Kessy na wachezaji wenzake
wapya, Vicent Andrew ‘Dante’, Juma Mahadhi na Beno Kakolanya kuwavaa MO
Bejaia.
Yanga iliwaongeza wachezaji hao hivi
karibuni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kinachoshiriki Kombe la
Shirikisho Afrika. Kessy aliyetokea Simba amekuwa ni kati ya mabeki bora
zaidi kwenye soka hapa Tanzania.
Timu hiyo, iliyopo kambini nchini
Uturuki itaavana na MO Bejaia keshokutwa Jumapili katika Uwanja wa Unite
Maghrebin mjini Bejaia, Algeria.
Akizungumza na Championi Ijumaa,
Ofisa wa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas,
alisema juzi jioni walipokea leseni za wachezaji hao kutoka Caf za
kuwaruhusu kucheza mechi hiyo hivyo mashabiki wa Yanga wasiwe na hofu.
“Jana (Jumatano) jioni tulipokea barua
Caf ikiwaruhusu wachezaji wanne waliosajiliwa na Yanga ambao majina yao
yalitumwa Caf kucheza mechi dhidi ya MO Bejaia.
“TFF tayari imeitaarifu Yanga kwa njia
ya barua kuwa ni ruksa kuwatumia wachezaji hao kama wakihitaji baada ya
kupokea baraka kutoka Caf.
“Majina ya wachezaji hao tuliyatuma hivi
karibuni kabla usajili huo haujafunguliwa na yalipitishwa na Caf baada
ya usajili huo kufunguliwa,” alisema Lucas.
Awali iliripotiwa kuwa wachezaji hao
hawawezi kucheza mchezo huo, lakini sasa TFF inamaliza utata huo ambao
ulishaanza kuwavuruga vijana wa Jangwani.
Tags
Michezo na burudani