"Mwenye Sifa za kumiliki silaha lazima awe na umri wa miaka 25 na kuendelea. Atafanyiwa uchunguzi huyu mtu kuangalia kama ana matukio ya uhalifu asiwe na tabia ya ugomvi wala historia ya matukio ili isije ikamdhuru yeye mwenyewe au jamii. Baada ya hapo atapewa hati ya tabia njema.
Baada hapo anapata Mafunzo kwenye Jeshi la Polisi katika Shirika la Uzalishaji Mali na kupata cheti baada ya hapo atakwenda kulipia silaha atapewa 'invoice'. Tunampa fomu 'N' za kuomba kumiliki silaha atajaza kopi Nne ataambanisha na cheti cha tabia njema na uwezo kutoka Jeshi la Polisi atakwenda hadi Serikali ya Mtaa au Kijiji watakaa na kuangalia tabia yake.
"Wakiridhika na historia yake watampitisha na kwenda ngazi ya Kata, wakishampitisha atakwenda kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya. Kikao atakaa OCD, Mkuu wa Usalama wa wilaya na Mkuu wa wilaya watamwita. Atahojiwa na kuangalia mapendekezo kutoka chini. Wakijiridhisha watayapeleka yale maombi Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa. Watakaa na baadaye watamwita.
"Akishakuwa na sifa zote atakwenda kununua silaha kwenye maduka mawili la Tanganyika Arms lipo Posta, Jijini Dar es Salaam na Mzinga. Bei ya Pistol kwenye Duka la Serikali la Jeshi (Mzinga Cooperation) ni Tshs Mil. 1.7 na Duka la Binafsi la Tanganyika Arms ni Tshs Mil. 4" Asp Charles Mburuma - Mrakibu Msaidizi Wa police.
0 Comments