Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

jinsi mahusiano yao yalivyoanza

​

Kwenye mahojiano mapya Priyanka Chopra(40) alipoulizwa ameeleza kuwa alianza kutongozwa na Nick Jonas(30) kupitia mtandao wa twitter mwaka 2016 ambapo alijitosa DM kumuomba namba ya simu mrembo huyo


Priyanka ameingia ndani kwa kueleza kuwa kipindi hicho alikuwa katika mahusiano serious ya muda mrefu na mwanaume mwingine kwa takribani miaka 6 ila alikuwa tayari anataka kuachana na mwanaume husika sababu hakuwa anaelewa mwelekeo.wa hayo mahusiano


Priyanka alimpa namba ya simu Nick Jonas baadaye wakawa wanachati ila akawa anasita kuanzisha mahusiano nae sababu ya wasiwasi wa kumpita umri wa miaka 10 pia hakutaka mahusiano ya kupotezeana muda sababu tayari akilini mwake alikuwa ashaamua kutaka kuingia katika ndoa na hatimaye kuanzisha familia


Kwa bahati wote Priyanka na Nick wakawa na marafiki wanaofahamika pande zote mbili ambapo pia Priyanka amesema marafiki zake wa karibu nao waliona mahusiano ya miaka sita aliyokuwa nayo kwa mwanaume mwingine hayana tija hayaeleweki  aachane nayo awe na Nick. Na kwa bahati kaka yake Nick anayeitwa Kevin nae akawa amemkubali Priyanka hivyo akawa kishawishi kizuri cha Nick na Priyanka kuwa wapenzi


Priyanka amesema baadaye akagundua Nick Jonas amepevuka sana kiakili na kimtazamo kuliko umri wake aliokuwa nao kipindi hicho hivyo wakawa pamoja rasmi 


2017 wakafanya public appearance pamoja katika MET Gala, baadaye wakachumbiana na kufunda ndoa mwishoni mwa 2018, na sasa wana mtoto mmoja


Kabla, katika mahojiano ya kipindi cha nyuma, Miss World huyo wa mwaka 2000 alipoulizwa baada ya kuwa wapenzi na Nick ni kitu gani kilimfanya azidi kumpenda Nick? ambapo Priyanka alijibu kwa kusema kuwa baada ya kufunga ndoa, kuna siku Nick alimueleza kuwa ataandaa chakula cha usiku wajumuike pamoja na marafiki wa upande wa Nick


Siku husika wakati wakielekea muda wa kujiandaa na dinner husika, Priyanka alipigiwa simu  ikimtaka aende sehemu kwa ajili ya mkutano wa ghafla wa kikazi, akiwa bado hajui ajibu nini na itakuwaje, mumewe akawa ameelewa simu inahusu nini ambapo alimjibu mkewe huyo kwa kumwambia kuwa japokuwa tumefunga ndoa naelewa kuwa kabla ya mimi kukutana na wewe tayari ulikuwa na ndoto na malengo yako makubwa na hadi kufikia sasa una mafanikio 


hivyo siwezi kukupangia kuwa fanya hiki au usifanye kile kwasababu wewe ni mtu mzima unajua kipi ni muhimu zaidi na kipi hakina uzito sana. Nick akaongeza kwa kumwambia sisi ni wanandoa ila bado kazi ni muhimu sana tena sana hivyo Priyanka aende kwenye mkutano wa kazi aachane na suala la mambo ya dinner party Nick aendelee na marafiki zake ikitokea siku nyingine watajumuika pamoja


Priyanka amesema baada ya kusikia maneno hayo ya mumewe alimshukuru Mungu kwa kumpa mume wa kipekee na kuahidi kuongeza upendo zaidi kwa mumewe sababu kabla, Priyanka alisema karibia wanaume wote aliowahi kuwa nao katika mahusiano walionekana wazi hawajiamini mbele yake wala kufurahia mafanikio yake kama mwanamke

Post a Comment

0 Comments