Nuh Mziwanda: Skendo za kijingajinga sasa basi

humph the GREAT

M SANII wa Bongo Fleva anayetamba kwa sasa na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa kwa sasa amechoka kutegemea skendo za kijinga kumng’arisha badala yake atajitahidi kuboresha kazi zake akiamini hiyo ndiyo njia pekee ya mafanikio.
Nuh aliyasema hayo alipokuwa akipiga stori na gazeti hili ambapo alisema kama ni skendo amefanya sana lakini matokeo yake anaona maendeleo yake kimuziki yanajongea kwa mwendo wa kobe suala ambalo ‘sometimez’ linamkatisha tamaa.
“Sasa nataka nikomae tu kwenye kazi yangu ya muziki, kiki za kijinga hazina faida, watu wanataka muziki mzuri tu na ndicho nitakachofanya ili niwakune mashabiki wangu,” alisema Nuh.


                                             nuhu mziwnda akiwa na shilole

 

Msanii huyo alipoulizwa kuhusu mahusiano yake kati ya yeye na shilole alikuwa hana mengi ya kuongea zaidi ya kusisitizia ni kwanini hapendi skendo kwani skendo nyingi chanzo cha kusambaa kwazo ni kuhojiwa hivyo hataki tena kuhojiwa kuhusiana ni nini hatima ya mahusiano yake kati yake na shilole
Previous Post Next Post