humph the GREAT
Mshambuliaji wa Klabu ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana alitangazwa kuwa mwanasoka Bora Ulaya baada ya kushinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu sasa.
Ronaldo alitangazwa kuwa Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kuwashinda wachezaji wenzke ambao ni Gareth Bale wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Wales pamoja na Antonio Greizman wa Athletico Madrid na Timu ya taifa ya Ufaransa ambapo klabu zao wote ni za Jiji la Madrid nchini Hispania.
Mshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya Norway Ada Hegerber ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa upande wa Wanawake 2015/2016

KURA
Katika Kura zilizopigwa na waandishi 55 wanachama wa UEFA katika Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya 2015/2016 matokeo yalikuwa.
Cristiano Ronaldo – 40
Antoine Griezmann – 8
Gareth Bale – 7
Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya mara tatu sasa huku. mara ya kwanza alishinda tuzo hiyo mwaka 2008 akiwa na Manchester United, pia akiwa na Real mwaka 2014.
Mshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya Norway Ada Hegerber ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa upande wa Wanawake 2015/2016
Bale alizungumzazjana wakati akihojiwa na WalesOnline: ‘Nilikuwa na bahati kushinda European Super Cup huko Cardiff na ilikuwa jambo la kushangaza kwangu, kwa familia yangu na marafiki pia.
‘Lakini Champions League ni levo nyingine kabisa. ni maalum kwa ajili ya Real Madrid tutaendelea kushinda tena na tena na kuwek historia kubwa juu ya hili.’
Baada ya kushinda tuzo hiyo jana, Ronaldo alisema: ‘Ni jambo la kushukuu. Wachezaji wenzangu wamekuwa nguzo kubwa ya mafanikio yetu kila mwaka. Ninafanya kazi kwa bidii na kujituma lakini bila wao isingewezekana.
Tags
Michezo na burudani