humph the GREAT
Ahamad Idd Fundikira akionesha jeraha enzi za uhai wake.
Dar es Salaam: Mwanajeshi mmoja, Ahamad Idd Fundikira aliyekamatwa kwa kosa la uhaini na utekaji akiwa mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kufungwa mwaka 1997, ameachiwa mwaka huu kisha kufariki dunia.
Kwa mujibu wa Idd Fundikira ambaye kwa sasa ni marehemu, alikuwa akifanya kazi kituo cha Mpanda kabla ya kukumbwa na hatia hiyo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 60 jela.
Baada ya hukumu hiyo alikata rufaa na kushinda akiwa tayari ametumikia kifungo cha miaka 17 gerezani baada ya mahakama kutomwona na hatia ya kosa la uhaini na kubaki na kosa moja la utekaji.
Hivyo aliendelea kutumikia kifungo kwa kosa la utekaji, katika Gereza la Ukonga lililopo jijini Dar es Saalam na baadaye kuhamishiwa Gereza la Rwanda mkoani Mbeya na ilipofika Julai 20, 2016 ndipo aliachiwa huru.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Ahamad Idd Fundikira
Kwa mujibu wa msamaria mwema aliyekuwa akiishi na kumlea marehemu baada ya kutoka gerezani aliyeombwa jina lake lisiandikwe gazetini, marehemu kabla ya mauti alionekana na kosa na kuhukumiwa kwenda jela kwa uhaini na utekaji akilalamikiwa kuingiza nchini wanajeshi kutoka nchini Burundi kitendo ambacho ni kinyume na sheria, wakati huo akiwa na cheo cha Luteni Kanali.
Msamaria huyo alisisitiza; “Tulihangaika kunusuru maisha yake kwa kujaribu kutafuta ndugu zake ambapo tulikwama japo marehemu alisema kabla ya kifungo chake aliacha watoto 13 na ndugu mwingine ambaye baada ya kutafutwa alisema hawezi kuhangaika na marehemu kwa sababu anayemjua yuko jela, hivyo tukakosa msaada wa ndugu zake hadi mauti yalipomkuta.”
Kaburi la ambamo mwili wa maehemu ulizikwa
Msamaria mwema huyo aliongeza: “Kwa kuwa alikosa ndugu basi waumini wa kanisa ndiyo walikuwa wanachanga michango kidogo na kunikabidhi hadi mauti yalipomkuta na hakuna ndugu yeyote aliyeshiriki msiba wake.”
Kwa mujibu wa msamaria mwema, marehemu hakuwa na kitambulisho au nyaraka iliyoonesha aliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ zaidi ya kombati aliyokuwa anapendelea kuivaa.
Marehemu alizikwa Julai 25, 2016 kwenye Makaburi ya Iganzo jijini Mbeya.
Ahamad Idd Fundikira akionesha jeraha enzi za uhai wake.Dar es Salaam: Mwanajeshi mmoja, Ahamad Idd Fundikira aliyekamatwa kwa kosa la uhaini na utekaji akiwa mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na kufungwa mwaka 1997, ameachiwa mwaka huu kisha kufariki dunia.
Kwa mujibu wa Idd Fundikira ambaye kwa sasa ni marehemu, alikuwa akifanya kazi kituo cha Mpanda kabla ya kukumbwa na hatia hiyo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 60 jela.
Baada ya hukumu hiyo alikata rufaa na kushinda akiwa tayari ametumikia kifungo cha miaka 17 gerezani baada ya mahakama kutomwona na hatia ya kosa la uhaini na kubaki na kosa moja la utekaji.Hivyo aliendelea kutumikia kifungo kwa kosa la utekaji, katika Gereza la Ukonga lililopo jijini Dar es Saalam na baadaye kuhamishiwa Gereza la Rwanda mkoani Mbeya na ilipofika Julai 20, 2016 ndipo aliachiwa huru.
Wakati akihukumiwa kwenda gerezani alikuwa na jeraha kubwa la kidonda kwa kile alichodai kuwa alipigwa na bomu akiwa kazini na kidonda hicho alidumu nacho miaka 19 akiwa kifungoni bila kupona hadi alipokumbwa na mauti Julai 23, 2016 akiwa jijini Mbeya.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Ahamad Idd FundikiraKwa mujibu wa msamaria mwema aliyekuwa akiishi na kumlea marehemu baada ya kutoka gerezani aliyeombwa jina lake lisiandikwe gazetini, marehemu kabla ya mauti alionekana na kosa na kuhukumiwa kwenda jela kwa uhaini na utekaji akilalamikiwa kuingiza nchini wanajeshi kutoka nchini Burundi kitendo ambacho ni kinyume na sheria, wakati huo akiwa na cheo cha Luteni Kanali.
Msamaria huyo alisisitiza; “Tulihangaika kunusuru maisha yake kwa kujaribu kutafuta ndugu zake ambapo tulikwama japo marehemu alisema kabla ya kifungo chake aliacha watoto 13 na ndugu mwingine ambaye baada ya kutafutwa alisema hawezi kuhangaika na marehemu kwa sababu anayemjua yuko jela, hivyo tukakosa msaada wa ndugu zake hadi mauti yalipomkuta.”
Kaburi la ambamo mwili wa maehemu ulizikwaKwa mujibu wa msamaria mwema, marehemu hakuwa na kitambulisho au nyaraka iliyoonesha aliwahi kuwa mwanajeshi wa JWTZ zaidi ya kombati aliyokuwa anapendelea kuivaa.
Marehemu alizikwa Julai 25, 2016 kwenye Makaburi ya Iganzo jijini Mbeya.
Tags
HABARI