TP Mazembe Yaichapa Yanga 3-1

humph the GREAT
Yanga
Kikosi cha Yanga kimeshindwa kufurukuta katika mchezo wake wa leo wa Kundi A kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1.
Mechi hiyo imepigwa katika Uwanja wa Stade de TP Mazembe, Lubumbashi.
TP-NA-YANGA
Mabao ya TP Mazembe yamewekwa kimiani na Bolingi (28), Kalaba (55) na (63) huku bao pekee la Yanga likifungwa na mshambuliaji Amissi Tambwe dakika ya 74.
Kwa matokeo ya leo, TP Mazembe imekaa kileleni mwa kundi hilo huku tayari ikiwa imeshajihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali ya michuano hiyo, huku Yanga ikiwa haina tena matumaini ya kusonga mbele.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post