HATIMAYE Polisi Waruhusu Wabunge Kufanya Mikutano Katika Majimbo yao

humph the GREAT
Jeshi la Polisi nchini limeruhusu mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa baada ya kuridhishwa na hali ya usalama nchini.

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya, amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu wa katiba.

“Maandamano na mikutano ya hadhara imezuiliwa hadi tathmini pana zaidi ya hali ya usalama itakapofanyika”, alisema.

Polisi imesema imeamua kuruhusu mikutano hiyo ya ndani baada ya kuridhishwa na mwenendo wa shughuli za kisiasa nchini huku akitoa wito kwa vyama vya siasa nchini na wananchi kuheshimu sheria za nchi na kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post