humph the GREAT
JERUSALEM Rais wa zamani wa Israeli bwana Shimon Peres (93), anaumwa ugonjwa wa kiharusi na madaktari wamesema ugonjwa huo umepelekea kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo.
Taarifa ya aina gani ya ugonjwa ndiyo inamsumbua kiongozi huyo imetolewa na daktari bingwa anayemtibu kiongozi huyo jana Jumanne.
Daktari Itzik Kreiss, mkurugenzi mkuu wa Sheba Medical Center, amewaambia waandishi wa habari nje ya hospitali hiyo iliyoko nje kidogo ya jiji la Tel Aviv kwamba:
“Ripoti inaonesha kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo hali hiyo imetokana na kiharusi na madaktari wetu tayari wamemweka kwenye chumba maalum.”
Mtoto wake wa kiume aitwaye Chemi amesema:
“Hali ya baba yangu ilikuwa mbaya sana lakini nawaomba ndugu zangu watulie wakati huu madaktari wanahangaikia matibabu yake”
“Baba yangu ni mtu muhimu kwangu. Namwangalia kwa jicho la tatu. Lakini kwa muda huu nafahamu yupo katika wakati mgumu”
Shimon Peres rais wa zamani wa Israeli
Baadaye ripoti ya madaktari imeeleza kwamba damu imesimama kuvuja kwenye ubongo na wamesema hawafikiri upasuaji masaa machache yajayo bali atawekwa chini ya uangalizi maalum.
Peres ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa kwenye siasa za nchi ya Israeli.
Amewahi kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha vipindi vitatu, Waziri wa fedha na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Israeli.
Mwaka 1994 alishinda tuzo ya amani ya Nobel kutoka na juhudi zake kubwa kutafuta suluhu na Wapalestina. alistaafu kama rais wa nchi hiyo mwaka 2014.Waziri mkuu wa sasa wa Israel Benjamin Netanyahu ametuma ujumbe kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook na kuandika:
“Shimon, we love you and the entire nation wishes you get well.”
Tags
HABARI
