humph the GREAT
Ule wimbo wa Weusi na Sauti Sol ambao umefanyika nchini Kenya
siku chache zilizopita unaweza ukasikika kabla ya mwaka huu kumalizika.
Japo
siku chache zilizopita alipoongea na Bongo5, Joh Makini alishindwa
kuweka wazi siku ambayo wimbo huo utatoka lakini kupitia akaunti ya
Instagram ya mmoja kati ya member wa kundi la Weusi, G-Nako ameweka
picha wakiwa na wasanii wa kundi la Sauti Sol na ameandika ujumbe ambao
unaweza ukawa unathibitisha kuwa wimbo huo utatoka kabla ya mwaka huu
kuisha.
“(E.A) WATU WA MUNGU IMESHAIVAA TAYARI NA MWAKA HAUISHII INAKUJA INSHALAAH!! ,” ameandika G-Nako kwenye mtandao huo.
Muda utaongea na tutajua kama ujumbe huo ulikuwa unatufahamisha kuhusu ujio wa wimbo huo au ni tofauti.
Tags
Burudani
