

N’gaya ambao mchezo wa kwanza walifungwa kwao Stade de Moroni kwa goli 5-1, leo wameingia uwanja wa Taifa na kujiuliza wamekosea wapi hadi kufungwa katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga, N’gaya leo wameilazimisha Yanga sare ya goli 1-1 huku wakitoa upinzania mkali.

Timu ya N’gaya ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli la kwanza baada ya kupiga shuti kali dakika ya 20 na kusababisha beki wa Yanga Vincent Bossou kujifunga na kuwafanya N’gaya waongoze mchezo hadi dakika ya 43 Haji Mwinyi alipoisawazishia Yanga kwa shuti la mbali alilopiga akiwa nje ya 18.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufuzu round inayofuata kwa jumla ya goli 6-2, huku safari ya N’gaya Club inaishia leo katika michuano ya Club Bingwa Afrika, kwa sasa Yanga atakutana na Zanaco FC ambayo imefuzu round inayofuata kwa kuitoa APR ya Rwanda baada ya kuifunga goli 1-0, baada ya mchezo wao wa kwanza uliyochezwa Zambia kumalizika kwa sare tasa 0-0.
0 Comments