Tamko la BASATA kuhusu ishu ya Nikki Mbishi na wimbo wa ‘I’m Sorry JK’

humph the GREAT



Kumekua na taarifa za kusitishwa kwa wimbo wa ‘I’m sorry JK‘ uliofanywa na Mwanahiphop Nikki Mbishi ambapo juzi aliandika kwenye Instagram yake kwamba ameitwa na baraza la sanaa Tanzania (BASATA).
Baada ya kutoka BASATA Nikki aliandika “Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa, hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria
Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia” – Nikki Mbishi

Baada ya maneno hayo Baraza la sanaa Tanzania leo (BASATA) limetoa tamko kupitia ukurasa wao wa Twitter na millardayo.com imelipata>>> “Nikki Mbishi aliitwa kwa mashauriano ya kazi za sanaa ambapo alibaini kwamba wimbo wa ‘I’m Sorry JK’ una kasoro, kaona ausitishe
Tunampongeza kwa kubaini mapungufu na kuchukua hatua stahiki, tunatoa wito wa kubuni maudhui yenye staha na yasiyo chonganishi” – BASATA

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post