humph the GREAT
KUNA watu wamezaliwa wakiwa na hofu kubwa ya kuwaogopa mademu wazuri.
Kuna mwingine akimuona demu mzuri mtaani, anajisemea kabisa kwamba; yule
si taipu yangu, eti kisa kapendeza, msafi na anaonekana matawi fulani
ya juu.
Mwanaume anatakiwa kujiamini, hakuna mwanamke duniani ambaye si saizi
yako, kila demu unayemuona mtaani basi jua kwamba huyo ni saizi yako
ndiyo maana Mungu kamuweka katika dunia hii na wewe kufanikiwa kumuona.
Leo nataka nikufundishe namna ya kumpata demu mkali, hata kama wewe ni
muoga, unahisi kwamba mademu wa aina hiyo si taipu yako lakini naamini
njia hizi zitakufanya kumpata kiurahisi kabisa na kufanya mambo yako,
kama ni kupanga naye maisha au la.
TAFUTA JINA LAKE KWANZA
Unapomtaka demu mkali mtaani kwako, kitu cha kwanza tafuta jina lake.
Hii itakusaidia kumshangaza. Wanawake wapo hivi, huwa hawapendi sana
kujulikana, inapotokea msichana huyo ukaonana naye na kumuita jina lake,
kwanza atasimama, atakuuliza umenijuaje? Nani kakwambia jina langu?
Usiogope, kwanza tabasamu, hilo litamfanya kuona kwamba wewe ni mtu
mzuri, jibu utakalompa, hakikisha linakuwa lile la kukutafuta baadaye.
Kwa mfano unaweza kumwambia: “Mbona nakufahamu! Wewe ni staa sana hapa
mtaani, kila mtu anakujua!” ukimwambia hivyo, atataka kujua zaidi na
zaidi, ni akina nani wanaomjua halafu mbona yeye siyo staa! Unachotakiwa
kufanya ni kujiweka bize, mwambie ‘nitakwambia nimekujuaje ila kwa sasa
kuna sehemu nawahi.’
Ukifanya hivyo itamfanya yeye kuwa na hamu ya kukutafuta. Hata
ukimwambia akutafute baadaye, atakutafuta kwa lengo la kutaka kujua
imekuwaje. Ukiona ameelekea kidogo, mwambie niachie namba yako,
nitakwambia, si hilo tu, kuna mengi kuhusu wewe.
Nakwambia hivi, kwa hatua hiyo, hakuna msichana ambaye atakukazia namba yake, lazima atakupa.
USIMLETEE SANA SHOBO
Akikupa namba, usijifanye kuwa na haraka ya kumtafuta. Unachotakiwa
kufanya ni kucheza na akili yake kwanza. Najua atakuwa na hamu ya kupata
simu yako, kwa siku hiyo mkaushie mpaka kesho yake ndipo umtafute. Kuwa
makini, usimpigie, wewe mtumie meseji, mwambie “Upo poa staa wangu wa
ukweli?” atakachokifanya ni kuuliza wewe nani! Inawezekana akawa anajua,
ila kwa mapozi ya kike ni lazima ajidai kuuliza. Mwambie ni yule
mshikaji wa jana! Ongezea kwa kumwambia kwamba utamtafuta ukirudi kutoka
kazini, hata kama huna kazi, jiongeze kidogo.
MPIGIE SASA, ANZA KUMSIFIA
Wanawake wanapenda sifa, wanapenda kusifiwa. Kitu cha kwanza mwambie
kwamba kuna siku uliwasikia washikaji wakimzungumzia, kwamba demu fulani
mkali, anajua kuvaa, ananukia vizuri, ukataka kumjua ndipo wakasema
kwamba ni yeye. Hilo litamfanya kujiona anakubalika sana, kumbe watu
wanamsifia mtaani, kumbe wewe unamuweka kwenye saiti yako.
Ukiwa unazungumza naye, jifanye mcheshi sana, mchekeshe, mwambie na wewe
ulivyokuwa na hamu ya kumjua msichana huyo msafi na mrembo ndiyo maana
ukaamua kumtafuta. Mpaka kufika hatua hiyo, ataanza kukukubali, kwa
ucheshi utakaomuonyesha atakuona wewe mtu mzuri na mtakuwa mnaanza
kuchati. Usimtongoze lakini muonyeshee dalili za kumtaka. Chati naye
hata kwa wiki moja halafu fanya njia ifuatayo;
MUOMBE MTOKO WA KIZUSHI
Hapa simaanishi mtoko wa kwenda klabu au ule mtoko siriazi sana, kwanza
mwambie wewe siyo mtu wa klabu ila unataka kumpeleka sehemu fulani hivi
kwenda kunywa kahawa au juisi. Kwenye kumuomba mwambie utajisikia furaha
ukiwa unatembea na demu mkali kama yeye, mwambie kila mwanaume
anajisikia fahari akitembea na msichana anayependeza na kunukia vizuri
kama yeye. Kwa sifa hizo za mara kwa mara, atakwambia anayo nafasi hivyo
atakukubalia.
KUWA MAKINI KWENYE MTOKO WAKO
Demu yeyote anapenda mwanaume mchangamfu, jinsi utakavyomuonyeshea
uchangamfu kwenye simu iwe hivyohivyo hata ukionana naye na kutembea
naye. Usimuonyeshee akahisi yule wa kwenye simu ni tofauti na huyu.
NENDENI MNAPOKWENDA
Usitake kutumia sana pesa, usitake kuingia gharama kubwa kwani mademu
wana kawaida ya kumsoma mwanaume siku ya kwanza tu. Kama vipi mwambie
wakati wa kurudi mtembee kwa miguu, hii itakupa nafasi ya kuzoeana sana,
hata kama akitaka mpande usafiri, mwambie mtachukua mbele, kwanza omba
kutembea naye hata nusu kilometa. Katika maongezi yote usijisifie ila
mfanye ajue unajua mambo mengi sana.
Jaribu kumwambia mambo ambayo unaamini hata yeye hayajui na angefurahi
kuyajua. Mwambie kuhusu hadithi ya Romeo And Juliet, mwambie kuhusu
Malkia Cleopatra alivyotetemesha kwa uzuri wake, mwambie mambo mengi
ambayo utaamini kwamba hayafahamu ila angependa ayafahamu.
MALIZIA KWA KUMWAMBIA HIVI…
Mkiachana na kurudi nyumbani, mpigie simu, mwambie unamisi uwepo wake,
ungetamani uwe naye tena, unaimisi harufu yake, mwambie ulikuwa karibu
na ua kwa hivyo ile harufu yake imekupata hata wewe. Mchekeshe kidogo,
mwambie unamisi tabasamu lake, mwendo wake wa twiga, mwambie unamisi
uzuri wake, yaani huo ndiyo muda wa kumsifia mpaka ajione duniani hakuna
mwanamke kama yeye. Ukifanya hayo, jua kwamba huyo mwanamke lazima
akukubali kwani atahisi yupo na mtu sahihi. Tukutane wiki ijayo kwa mada
nyingine bomba zaidi.
Tags
Je wajua ?