humph the GREAT
Baada ya kusubiriwa kwa hamu mchezo wa fainali ya FA Cup kati ya
Arsenal dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Wembley, hatimae May 27 2017
mchezo huo ambao ulikuwa unatajwa kama ndio utaamua hatma ya kocha
Arsene Wenger ndani ya Arsenal ulichezwa rasmi.
Licha ya Arsenal hivi karibuni wamekuwa wakionekana hawafanyi vizuri,
wamefanikiwa kuchukua taji lao la 13 la FA jana na kuwa club
inayoongoza England kutwaa taji hilo mara nyingi zaidi ikifuatiwa na Man
United waliyowahi kutwaa taji hilo mara 12.
Arsenal imefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 magoli ambayo
yalifungwa na Alex Sanchez dakika ya 4 na Aroon Ramsey dakika ya 79
ikiwa ni dakika 3 zimepita toka Diego Costa aifungie Chelsea goli la
kwanza, ushindi sasa unamuwekea rekodi Arsene Wenger wa kuwa kocha pekee
aliyewahi kutwaa mataji 7 ya FA katika historia ya Kombe hilo.
0 Comments