Jinsi wastara alivyotetemeka akipokea hela ya magufuli

humph the GREAT

Msanii wa Bongo Muvi, Wastara Juma, amesema kuwa hakuamini baada kupigiwa simu na Rais John Pombe Magufuli ili kumjulia hali na kumsaidia kiasi cha fedha kwa ajili ya matibabu ya mguu wake.
“Nilishangaa sana kuona Rais Magufuli ameikariri sauti yangu, kwa sababu alivyonipigia simu alipokea mdada wangu na alivyoanza kuongea nae tu akagundua kuwa sio mimi ndipo alipomuagiza aniletee simu nikaongea nae.
“Rais Magufuli ni mkali hata wakati nilivyokuwa naongea nae nilikuwa natetemeka sana ila namshukuru kwa kuguswa na matatizo yangu, kwakweli ni Rais ambaye anasaidia watu wengi,” alisema Wastara wakati akipokea msaada wa Sh. milioni 15 kutoka kwa Rais Magufuli na mkewe mama Janeth.

FUATILIA TUKIO HILO

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post