Diamond na hamisa wayamaliza kuhusu kumlea mtoto

humph the GREAT

Diamond na Hamisa Mobetto Waamua Kwa Pamoja Kumlea Mtoto Wao..Wayamaliza Mahakamani

Sakata la matunzo ya mtoto lilikuwa kikiwakabili mastaa wawili Naseeb Abdul ‘Diamond’ na Hamisa Mobeto leo liliingia Mahakakama ya Kisutu jijini Dar kitendo cha Ustawi wa Jamii upande wa watoto ambapo wanahabari hawakuruhusiwa kuingia kusikiliza majadiliano hayo.

Hata hivyo baada ya kumaliza majadiliano hayo Diamond alisema kikao hicho kilihusu malezi ya mtoto ambapo alisema wamekubaliana yeye na Mobeto kama wazazi washirikiane kumpa malezi bora mtoto huyo kwa faida yao wenyewe.

Diamond amesema mtoto huyo ni wake hilo halina mjadala hivyo ni lazima ampe matunzo bora ingawa alisema awali Mobeto alikuwa akishawishiwa na baadhi ya watu amkomoe kupitia mtoto huyo ingawa hilo sasa limewekwa sawa. “Nitamlea mwanangu” Alimaliza kusema Diamond.

Mobeto upande wake naye alisema kuwa suala la malezi ya mtoto huyo wameshalimaliza hivyo hakupenda kuongea zaidi na kuingia ndani ya gari alilokwenda nalo na kumuacha Baba Mtoto wake huyo viwanja vya mahakama hiyo
Angalia hapa

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post