MKONGWE wa Bongo Fleva aliyetamba miaka ya 2000 kwa staili yake ya Takeu, Lukas Mkenda ‘Mr Nice’ amefunguka na kuwaasa wasanii wenzake kuimba vitu vyenye msingi ili wasipotishe mashabiki wao wanaowatazama.
Mr Nice ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kupeleka orodha ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambazo zina maudhui yaliyo kinyume na Kanuni za Huduma ya Utangazaji ya mwaka 2005.
“Ninachoweza kusema bila kuficha, vijana na watoto wadogo ndiyo wanaopenda muziki sasa hivi, hivyo msanii atakapoimba kitu kisicho na maana, adabu wala mantiki, atakuwa anampotosha mtoto. Maana vijana wanaosikiliza na kutazama muziki wetu wengine husema natamani kuwa kama msanii fulani bila ya kujua mtu huyo anaimba matusi matupu ‘so’ unategemea nini hapo”, amesema Mr Nice
0 Comments