Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

KUKOMESHA KISUKARI NI MIMI NA WEWE

humph the GREAT




Ndugu msomaji nikukaribishe tena katika mwendelezo wa makala haya ya ugonjwa hatari wa kisukari kwa leo tukiangazia athari kubwa zinazowezasababishwa na kisukari karibu.

TULIPOISHIA MAKALA YALIYOPITA
Kwani kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani(WHO)inadai magonjwa yasiyo ya kuambukiza ndio chanzo kikubwa cha vifo duniani yakifanya ongezeko ya vifo vyote kwa kila mwaka.
Inakisiwa kuwa mwaka wa 2020 magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza yatasababisha asilimia 73 ya vifo vyote duniani na asilimia 60 ya ukubwa wa tatizo la magonjwa duniani.
SONGA MBELE ZAIDI..............

Kutokana na kuwepo kwa athari mbalimbali ambazo husababishwa na ugonjwa huu usiowa kuambukiza wa kisukari ni pamoja na kuwepo kwa uwezekano mkubwa kwa mgonjwa aliyekwisha kuathiriwa na kisukari wenda akapatwa na tatizo la figo .Japo ni vigumu kujua ni mgonjwa yupi wa ugonjwa wa kisukari anawezakukumbwa na tatizo hili la figo japo zipo ishara kadha wa kadha.
Ieleweke kuwa ugonjwa huu wa kisukari ni chanzo kikuu cha ugonjwa wa figo ulio katika hatua ya mwisho kutokana na walio wengi hupatwa na tatizo hili ,hata hivyo kwa mgonjwa wa kisukari ni vigumu sana kupatwa na tatizo la figo hasa katika kipindi cha miaka kumi ya kwanza kabisa ya tatizo la ugonjwa wa kisukari.
Ikumbukwe kuwa ugonjwa huu wa kisukari huorodheshwa na shirika la afya ulimwenguni kuwa ni moja ya sababu kuu za watu kufariki mapema ikiwa ni pamoja na kupatwa na matatizo ya upofu,figo kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa ,mtu kukatwa mguu na kupatwa na ugonjwa wa kiharusi,kwani hali hii yote huchochea athari kubwa za kiuchumi hasa kwa mtu na hata familia kwa ujumla.
WHO katika kuangazia athari ya tatizo la ugonjwa huu hatari wa kisukari hasa kwa jamii za kimataifa katika kusaidia kinga uchunguzi na usimamizi unaotakiwa kwa ugonjwa huo ambao ulisababisha vifo vya takribani watu milioni 1.6 kwa mwaka 2016 pekee kote ulimwenguni.
Kuendelea kujitokeza kwa matatizo mbalimbali hasa haya yote huchochewa na kuwepo kwa tatizo hili la kisukari ambalo limekuwa tishio kubwa kwa maisha ya wanajamii mabalimbali,hata hivyo jitihada za haraka zinatakiwa kuendelea kuchukuliwa kutokana na hali halisi ya tatizo kuendelea kushika kasi kwa kuenea ulimwenguni kote.
Aidha, athari kubwa ya kiuchumi itokanayo na ugonjwa huu wa kisukari kuna uwezekano mkubwa kutokea kwa mtu yeye mwenyewe na familia kwa ujumla kwani gharama hiyo ya kupanda hali ya maisha yawezasababishwa na sindano ya Insulini na ufuatiliaji pekee ambao waweza kutumia nusu ya mapato kwenye familia hali inayowafanya walio wengi kushindwa kupata dawa za kisukari mara kwa mara na huduma husika hali inayochochea tatizo kubwa na kuendelea kuongeza idadi ya walioathiriwa na ugonjwa hatari wa kisukari.
Kutokana na tatizo hili kuendelea kushamiri na kuwa kubwa kwa kiasi chake hali inayoendelea kuleta athari kubwa kwa jamii ya kitaifa na kimataifa kwani ni wakati sasa kwa kila mmoja wetu kutambua ugonjwa huu kwa undani ikiwa ni pamoja na kufuatilia ushauri wa kitaalamu kuhusu afya yako ili kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ugonjwa huu ikiwa umebainika kuathiriwa.
Daktari mgeta anaeleza kwa ujumla jinsi ya kuepukana na tatizo hili kwa kuchukua tahadhari mapema ikiwa ni pamoja na jamii kuwa na utamaduni wa kujali afya kwa ujumla hapa anasema;
"Kwa ujumla jamii ijipe mtazamo wa kuwa inapima na kuchunguza afya baada ya muda fulani hasa baada ya mwezi unapashwa kuangalia afya yako kwa ujumla,pia mazoezi yapewe kipaumbele sana hali itakayoufanya mwili kuwa na kiwango cha sukari iliyo na uwiano sawa" alisema Mgeta.
Kutokana na hali halisi ya mambo yanayozidi kujitokeza kwa kasi sana kutokana na kuwepo kwa tatizo hili la ugonjwa wa kisukari ni hakika kwa pamoja kushirikiana kwa kiasi kikubwa na kwa nguvu moja katika kulitokomeza tatizo hili.licha ya tatizo hili kuendelea kuwa pana na lenye nguvu katika kukatiri uhai wa maisha ya watu walio wengi ulimwenguni wewe na mimi bado tunayo nafasi ya kutumia dawa katika kuondokana na hilo tatizo ikiwa ni pamoja na kuendele kuchunguza afya zetu kwa pamoja.

Post a Comment

0 Comments