MBUNGE wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali amelieleza Bunge,
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe hakushambuliwa na watu
wasiojulikana bali alidondoka katika ngazi akiwa amelewa. Amewatuhumu
Chadema, kucheza michezo ovu dhidi ya Serikali.
“Jana
limetokea jambo, Msigwa Peter anasema jana mpaka saa 3 walikuwa kwa
Mwenyekiti na baadaye akatoka, walienda kunywa Pombe, walienda kulewa na
hata tukio sisi tunajua Mh. Freeman Mbowe kapanda ngazi kateleza
kavunjika, huu ni ukweli kabisa.
“Hivi
inawezekanaje KUB atembee usiku wa manane bila ulinzi na ni chama
chenye umakini, mnasema hizi ndiyo akili mbadala, tungekaa kimya ila kwa
sababu wameisingizia Serikali eti wameshambuliwa Kisiasa, mtu anataka
akuzuie uchaguzi akuvunje leo.
“Watanzania
naomba mfahamu hii michezo inafanyika na ukitaka kujua kama ni usanii,
kwa nini kaenda Ntyuka na siyo General Hospital, kwa sababu alijua akiwa
Serikalini pale watasema alikuwa amelewa, ninavyoongea saa hivi Ntyuka
pale hayupo keshakimbia tayari,” amesema Lijualikali.
0 Comments