MWIGIZAJI nguli wa vichekesho Bongo,
Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’, ameibuka na kuonesha pesa na utajiri wake
anaomiliki uliotokana na kazi yake hiyo ya kuvunja watu mbavu.
Akizungumza
na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Kingwendu amesema kuwa, sanaa yake imempa
mafanikio makubwa, kwani anamiliki vitu vya thamani kutokana na kazi
yake hiyo.
“Mimi
ninamshukuru sana Mungu, tangu nilipotoka mpaka nilipo sasa, kwani
nimepata mafanikio makubwa; nini magari? Nyumba ninazo, nimejenga nyumba
kubwa tu maeneo ya Mbagala, namiliki magari matatu; Toyota Crown (Paka
Mweusi) ambayo imenigharimu Sh milioni 25, Toyota Prado Old Model, kwa
sasa liko Arusha kwa ajili ya kusafirisha watalii, Toyota Noah,
bodaboda, saluni mbili na duka.
“Nina mpango wa kufungua kampuni yangu mwenyewe kupitia jina langu la Kingwendu.
“Pia kwa sanaa yangu nimeweza kusomesha watoto. Hayo ndiyo mafaniko ninayojivunia.
“Namshukuru
sana Francis Ciza (Majizo) ambaye ni Mkurugenzi wa E-FM, kwani
amenisimamia sana katika kazi zangu. Hata wazo la kwenda kutangaza pale
kwenye redio yake (E-FM), yeye ndiye alitoa hilo wazo, maana nilienda
katika kipindi tu kama mgeni, ndani ya mwezi mmoja, wakawa wananipa
majaribio ya kusoma magazeti nikiwa na Steve Nyerere. Majizo na
wafanyakazi wake wakaona kipaji changu, nikabaki kuwa kama mtangazaji
mpaka sasa,’’ amesema Kingwendu.
Kingwendu amesema kuwa, wasanii wengi wamekuwa wakijisahau sana kwa kufanya starehe na si maendeleo.
“Wasanii wamekuwa wakikimbilia kuanza kununua magari badala ya kujenga kama jinsi nilivyofanya,” amesema Kingwendu.
Kingwendu
ni mwigizaji wa vichekesho ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia
kazi zake. Amecheza filamu nyingi akiwa na wachekeshaji wakali hapa
Bongo.
0 Comments