Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ticker

6/recent/ticker-posts

BEI MPYA ZA MAFUTA

humph the GREAT

 

Kwa mujibu wa Jedwali Na. 1, bei ya rejareja kwa petroli ni Sh 2,877 kwa lita Dar es Salaam, Sh 2,938 Tanga, na Sh 2,969 Mtwara. Kwa dizeli, bei ni Sh 2,767 Dar es Salaam, Sh 2,828 Tanga, na Sh 2,859 Mtwara. Mafuta ya taa yatauziwa Sh 2,629 Dar es Salaam, Sh 2,690 Tanga, na Sh 2,722 Mtwara.

Katika Jedwali Na. 2, bei kikomo za jumla kwa petroli ni Sh 2,735.79 Dar es Salaam, Sh 2,743.07 Tanga, na Sh 2,743.94 Mtwara. Kwa dizeli, bei ni Sh 2,625.66 Dar es Salaam, Sh 2,640.23 Tanga, na Sh 2,641.85 Mtwara. Mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 2,489.14 kwa jumla Dar es Salaam, huku Tanga na Mtwara hakukuwa na mabadiliko.

EWURA imeeleza kuwa bei hizi mpya zimezingatia gharama za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia, ambazo zimepanda kwa asilimia 6.8 kwa petroli, asilimia 9.3 kwa dizeli, na asilimia 8.1 kwa mafuta ya taa. Pia, gharama za kuagiza mafuta (premiums) kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 27.98 kwa petroli na asilimia 8.04 kwa dizeli, huku gharama hizo zikishuka kwa asilimia 5.64 kwa mafuta ya taa. Hakukuwa na mabadiliko ya gharama hizo katika bandari za Tanga na Mtwara.

Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa bei za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya, na mikoa mingine zitaainishwa katika Jedwali la 3. Taarifa hii ni muhimu kwa watumiaji wa nishati nchini ili kujipanga kifedha na kufuatilia mwenendo wa bei za mafuta kwa uangalifu

Post a Comment

0 Comments