Youtube kumlipa trumph





Kampuni ya YouTube imekubali kulipa dola milioni 24.5 ili kusuluhisha kesi iliyofunguliwa na Rais wa Marekani Donald Trump kutokana na kitendo cha kampuni hiyo kuifungia account yake kufuatia ghasia za Januari 6, 2021 katika majengo ya Congress. 

 Kwa hatua hiyo, YouTube imekuwa Kampuni ya mwisho kati ya Kampuni tatu kubwa za teknolojia ambazo Trump alizishtaki Mahakamani ikiwemo Meta na Twitter (sasa ikijulikana kama X) kufikia makubaliano ya kifedha kuhusu suala la kufungiwa kwa account zake kwenye majukwaa yao.

 Nyaraka za Mahakama zimeonesha kuwa katika ya malipo hayo ya Youtube, dola milioni 22 zitaelekezwa kwenye Taasisi isiyo ya kiserikali ya Trust for the National Mall inayojihusisha na kuhifadhi na kuendeleza eneo la kihistoria la National Mall na kusaidia ujenzi wa White House State Ballroom huku dola milioni 2.5 zikilipwa kwa Walalamikaji wengine wakiwemo American Conservative Union. 

 Trump kupitia ukurasa wake wa Truth Social alijigamba kwa matokeo hayo akisema “Ushindi huu MKUBWA unathibitisha kuwa udhibiti wa Big Tech una madhara.” Kabla ya hapo Meta ilikubali kusuluhisha kesi hiyo kwa malipo ya dola milioni 25 mwezi Januari 2025 huku X ikilipa takribani dola milioni 10 mwezi Februari mwaka huu. Majukwaa hayo ya kijamii yaliamua kumsimamisha Trump kwa madai kwamba machapisho yake kuhusu ghasia za Capitol yalihatarisha kuchochea vurugu zaidi.

Na baada ya kuhitimisho hilo trumph akatoa tamko na katazo kubwa ambalo liliwalenga sana wale wote wanamiliki mitandao hiyo ya kijamii na baadhi ya mitandao mengine ambayo huenda kwa namna moja au nyingine angetumia, kuwa kufungia account ya mteja wao ilhali hawajafanya uchunguzi wa kutosha haitakiwi la si hivyo wasiruhusu kirhisi watu kujiunga na mitandao yao

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post