No title





Mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la kalenga, Iringa vijijini, kupitia tiketi cha chama cha mapinduzi(CCM), Godfrey mgimwa akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho, katika ofisi ya ccm mkoa wa iringa kwa shagwe kubwa baada ya kutangazwa matokeo yaliyo rasmi. Chama cha mapinduzi(CCM) kimeibuka na ushindi wa kishindo kutoka kwa apinzani wao chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA).

*************************************************

Matokeo ya uchaguzi jimbo la kalenga Iringa vijijini, yametangazwa rasmi na tume ya taifa ya uchaguzi mjini Iringa, kuwa chama cha CCM kilipata jumla ya kura 22962 na chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Kilipata kura 5853, na chama cha CHAUSTA kilipata jumla ya kira 150. Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia 79.4, CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5. Matokeo hayo ni ya jumla kwa kata 13 za jimbo hilo


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post