YANGA WAPATA AJALI MIKESE, MORO


Basi la Yanga likiwa mtaroni eneo la Mikese, Morogoro.

Kikosi cha Yanga SC kimepata ajali baada ya basi lao kutumbukia mtaroni katika eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Basi hilo limepata ajali likitokea mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jana.
Taarifa zinasema hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post