TUNDAMAN AMBADILI MASOGANGE

Stori: Humphrey Eno

KIBAO cha Msambinungwa cha mkali wa Bongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tundaman’ kimegeuka mwiba kwa Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye ameuza sura kupitia video ya wimbo huo, kwa sababu watu mitaani wameacha jina lake halisi na kumwita Msambinungwa.

Khalid Ramadhan ‘Tundaman’.

Akisebeza na Stori Mix, Tundaman alisema, maana ya jina la kibao chake hicho ni mwanamke ambaye hajatulia – mapepe na ameshaelezea maana hiyo kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ndiyo maana Masogange anachukizwa anapobadilishwa jina na kupewa hilo.
“Masogange ameshanipigia simu mara nyingi  akinilalamikia kuitwa hilo jina. Sikuwa na nia mbaya na wala sikumlenga yeye.

Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Ajue kuwa pale alivaa uhusika usio wake, si kweli kuwa tabia zilizoelezwa kwenye kibao hicho ni zake. Watu waache kumuita hilo jina na yeye pia aachane na maneno ya watu.”

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post