NI mwanamke mrembo kupindukia, kwa matendo yake anaweza kuitwa mzimu na pia mtakatifu, zote ni sifa zake. Mwanamke huyu si mwingine bali mtawa aitwaye Sista Karen kwa saa kumi na mbili lakini kwa saa nyingine kumi na mbili za siku, jina lake ni Milembe, muuaji asiye na huruma.
Amekamatwa na polisi akijiandaa kwenda darasani kufundisha wanafunzi wake somo la Biashara, ingawa ni siku ya sikukuu ya Krismasi, wanafunzi wake walimpenda kwa moyo wa kujitolea bila kujua upande wake wa pili alikuwa ni mtu wa namna gani.
Anafungua mlango na kukutana na midomo mitano ya bunduki ikiwa imemwelekea, mwili wake unatetemeka, anaamriwa kwamba yupo chini ya ulinzi, akiitwa muuaji mkubwa aliyejificha kwenye vazi la Kitawa.
Je, mwanamke huyu ni nani? Ni kwa nini anaitwa mzimu na mtakatifu? SONGA NAYO…

“Kaa chini!” askari mmoja aliamuru akimpiga sista Karen na kitako cha bunduki, akapasuka chini ya jicho na damu kumtoka zikilowanisha mavazi yake ya kitawa.
Akaporomoka na kuketi chini, mwili wote ukitetemeka.
“Kosa langu ni nini?” hakuna askari aliyemjibu, ni kweli hakuwa na kumbukumbu ya kilichotokea zaidi ya kujikuta ana nguo zenye damu, ambazo aliamua kuzichoma kupoteza ushahidi.
“Muuaji mkubwa wee!” askari walizidi kumwita jina ambalo hakuelewa maana yake.
“Nimemuua nani?”
“Utajieleza hukohuko kituoni.”
Akapigwa pingu mikononi na askari wakazama ndani ya nyumba yake wakipekua kila kona, haukupita muda mrefu sana mmoja wao akaibuka akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na fuvu la mwanadamu! Watu wote wakabaki midomo wazi, waliokuwa na shaka kwamba Sista Karen alikuwa muuaji, akiwemo mwalimu mkuu wa shule hiyo, Padri Andrew Karugendo, walibaki midomo wazi.
“Sista! Nini tena hiki? Fuvu la mwanadamu ni la nini?” mkuu wa shule aliuliza akijifuta machozi.
“Hata mimi sielewi, nahisi hawa askari wamekuja nalo, hii ni njama padri!”
“Paaa!” ulikuwa ni mlio wa kibao kikitua kwenye shavu la kushoto la Sista Karen, askari alifoka ni kwa nini alikuwa akisingizia Jeshi la Polisi mambo ambayo anajua siyo kweli.
“Nyamaza!”
Akanyanyuliwa na kuanza kusukumwa kwenda nje ambako wanafunzi wote wa Shule Sekondari ya St. Magdalena, iliyomilikiwa na Kanisa Katoliki walikuwa wamekusanyika kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, badala ya kwenda kanisani kwenye ibada ya Krismasi.
Hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba mwalimu wao kipenzi, rafiki wa kila mwanafunzi, mpole na mkarimu ambaye alikuwa tayari hata katikati ya usiku umwamshe aje kukufundisha na akakubali ndiye alikuwa amekamatwa kwa mauaji.
“Wanamwonea!”
“Wooooo! Woooo! Wooooo!” wanafunzi walikuwa wakizomea wakati askari wakiondoka na sista kuelekea kwenye magari, baadhi ya wanafunzi na hata walimu walionekana wakilia.
“Msilie, nitarudi!” alisema sista Karen akiwa kwenye gari.
Muungurumo wa magari ukasikika yakitimua vumbi kuacha mazingira ya shule, moja wapo kwenye magari hayo likipiga king’ora na askari wenye bunduki zilizowekwa tayari wakining’inia juu ya magari hayo tayari kwa lolote, picha ilikuwa ikionekana kama vile askari wa Marekani walikuwa wamemkamata Osama bin Laden.
Njia nzima, Sista Karen alikuwa akilia, hakuelewa kabisa ni kitu gani kilikuwa kimetokea, ni kweli alijikuta ana mabaka ya damu kwenye nguo zake na kuamua kuzichoma ili kupoteza ushahidi lakini alipojiuliza damu zile zilikuwa ni za nani hakuwa na jibu. Kituoni alishushwa na kusukumwa huku akipigwa hadi ndani ya mahabusu ambako alifungiwa.
“Nimefanya nini?” alijiuliza bila kupata jibu.
Nusu saa baadaye, lango la chuma lililokuwepo mahabusu lilifunguliwa, Sista Karen akiwa hana tena kilemba kichwani akaburuzwa na kupelekwa kwenye moja ya vyumba vya mahojiano.
Huko alimkuta mwanaume mmoja wa Kizungu akiwa na askari polisi mwenye nyota nyingi mabegani, wote wakamwangalia kwa hasira.
“Is this the one?” (Ni huyu?)
“Yeah! Very simple and externally she looks innocent!” (Ndiyo! Mtu wa kawaida na kwa nje anaonekana ni mtu asiyekuwa na hatia!)
“But she is lethal murderer!” (Lakini ni muuaji hatari!)
“Who did I kill?” (Nimemuua nani?)
“Khu!” ulikuwa ni mlio wa buti la polisi likimkanyaga sista Karen kichwani, ukifuatiwa na maneno: “Shut up! Unamjibu afande?” kutoka kwa askari aliyemburuza kumwingiza chumbani.
“Chukueni maelezo yake kisha upelelezi uanze, utakapokamilika afikishwe mbele ya sheria haraka iwezekanavyo, ameliaibisha sana taifa, mwanamke unafanya vitendo vya namna hii? Tena mtawa? Hii ni aibu kubwa na hata kwa kanisa lako.”
“Sijafanya kitu chochote kibaya,” alisema Sista Karen na kuendelea kulia.
***
Habari za mtawa kukamatwa zilikuwa zimetapakaa kila mahali, vyombo vingi vya habari vya kuandika na vya kielektroniki vilikuwa vinatangaza juu ya Sista Karen mfululizo, kama vile ilikuwa ni habari ya mapokezi ya kiongozi mkubwa duniani mithili ya papa au Rais wa Marekani na kuwafanya maelfu ya watu wamiminike kwenda kituo cha polisi cha kati ambako alikuwa ameshikiliwa wakitaka kumwona.
Polisi walikuwa na kazi ya kuwadhibiti watu waliojaa kama vile kulikuwa na tamasha, barabara za Sokoine na Kilwa zilikuwa zimefungwa, hakuna hata gari moja lililopita kwa jinsi umati wa watu ulivyokuwa mkubwa. Tukio hilo lilikuwa limechukua masikio yote ya Watanzania.
“Hebu rudisha nyuma!” ilikuwa ni sauti ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Robert Msigwa ambaye alilazimika kuwaita askari wote wa kituo cha kati ofisini kwake ili waweze kujadiliana juu ya tukio hilo ambalo lilichukua sura ya kimataifa.
Mkanda ndani ya kamera ya CCTV ukarudishwa nyuma na kuanza kuachiwa uende tena mbele taratibu, wote wakiangalia kwa makini, alikuwepo pia Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Bwana Nzungu Baliza, wakihakikisha hakuna kosa lolote lililofanyika, mwisho wa kuangalia mkanda huo walithibitisha kabisa waliyemkamata ni mtu sahihi, kwani ilikuwa ni sura ya Sista Karen akiwa hajavaa nguo za kitawa.
“Ni yeye!” mkuu wa jeshi la polisi alisema.
“Hilo halina ubishi afande, cha muhimu ni kuchunguza tu ni sababu ipi iliyomfanya aamue kuua mtu na baadaye kufukua kaburi la Wajerumani kisha kuondoka na fuvu.”
“Basi fanyeni hivyo.”
“Pia kuna kisu alichofanyia mauaji, alikiacha hapohapo!”
“Chukueni alama zake za vidole, mlinganishe na mtakazozikuta kwenye kisu! Au alikuwa amevaa mipira mikononi?”
“Hapana, hivi sasa zoezi la kuchunguza alama za vidole ndiyo linaendelea!”
“Tunaweza kupata majibu ndani ya muda gani?”
“Dakika arobaini na tano.”
”Basi tusubiri ili tuwe na uhakika, katika kosa kama hili hatutakiwi kuhisi vitu lazima tuwe na uhakika.”
“Sawa afande!”
Upande wa pili kwenye kituo cha kati ambako maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika, Sista Karen alikuwa akifanyiwa mahojiano na Inspekta wa Polisi, Mary Nchimbi, mwanamke mpole, makini na Mchamungu ambaye alihakikisha kila kitu kinafanyika ipasavyo bila chembechembe ya ugandamizaji wala unyanyasaji.
“Kwa hiyo jana saa tatu usiku ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa chumbani kwangu, baada ya kuwa nimemaliza kufundisha wanafunzi somo la Biashara.”
“Hukutoka sista?”
“Sijatoka.”
“Una uhakika?”
“Ndiyo.”
Mlango ukafunguliwa, akaingia askari mmoja na kifaa cha kuchukulia alama za viganja vya mikono, Sista Karen akaamriwa atandaze viganja vyake juu ya kifaa hicho, zoezi lilipokamilika askari huyo aliondoka na kuwaacha wakiendelea na mahojiano.
“Lile fuvu unalitambua?”
“Nimeshangaa mno kukutwa na fuvu, sina uhusiano nalo kabisa, mimi ni mtawa na fuvu wapi na wapi dada yangu?”
“Lakini limekutwa chumbani kwako?”
“Kuna mtu kati ya askari waliokuja ndiye amelileta.”
“Unafikiri ni kwa nini afanye hivyo?”
“Uadui umetambaa sana hapa duniani kwa hivi sasa, watu hatupendani, kila mtu anatafuta sababu ya kumkwamisha mwenzake, kwani hujawahi kusikia habari za watu waliowekewa madawa ya kulevya nyumbani kwao? Au mikono ya albino na noti bandia ili tu waingie hatiani na kufungwa?”
“Ni kwa nini mtu akufanyie hivyo wewe?”
“Sijui.”

Je, nini kitaendelea? Fuatilia siku ya Jumatatu katika Gazeti la Ijumaa Wikienda.
Tags
Hadithi & Simulizi