Maisha yake yamegubikwa na siri kubwa ambapo hakuna anayeweza kujua chochote kutokana na mwonekano wake usio na hata chembe ya dosari. Kwa kumtazama anaonekana mpole, mnyenyekevu na mtiifu huku urembo wake nao ukizidi kuficha siri kubwa iliyokuwa imejificha nyuma yake.
Msichana huyu mrembo ana uwezo wa ajabu wa kubadilika kutoka hali moja kwenda nyingine bila mtu mwingine yeyote kujua kinachoendelea. Akiwa katika ulimwengu wa kwanza, anaitwa Karen na anaishi maisha ya utakatifu wa hali ya juu, akiwa ni mtawa.
Hali ni tofauti kabisa katika ulimwengu wa pili ambapo anabadilika na kuwa mtu mwingine tofauti, jina lake likiwa ni Milembe. Akiwa katika hali hii, anakuwa na roho mbaya kupita maelezo na anaishi kama mzimu, akielekezwa nini cha kufanya na sauti ambayo haijui ni ya nani.
Karen yupo kwenye chuo cha watawa kilichopo Tosamaganga anakoendelea kuzusha hali ya sintofahamu kila kukicha. Ameshatumiwa katika mazingira ya kutatanisha kutekeleza kifo cha mtawa wa kwanza, Isabela.
Anajaribu kwa mara nyingine kutoroka lakini katika hali ambayo hata mwenyewe haijui, anajikuta akihusika pia katika tukio lingine la kutisha, kiasi cha kumfanya mkuu wa chuo aanze kumtilia shaka.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…
Mkuu wa chuo alipofika kwenye mlango wa chumba cha Karen, aligonga mlango mfululizo lakini hakuitikiwa. Akajaribu kuutingisha mlango lakini akagundua kuwa haukuwa umefungwa, akausukuma na kuingia ndani huku akimuita Karen.
Licha ya kuita kwa sauti kubwa zaidi ya mara tatu, bado hakukuwa na jibu lolote, ghafla akasikia kishindo kikubwa bafuni kilichomshtua kupita kiasi.
“Karen! Karen!” mkuu wa chuo aliita tena lakini hakuitikiwa, kwa mbali akaanza kusikia bomba la maji lililokuwa bafuni humo likifunguliwa na kuanza kumwaga maji. Akajua kuna mtu alikuwa anaoga.
“Sasa kwa nini haniitikii? Ina maana hajasikia? Na kile kishindo ni cha nini?” Mkuu wa chuo alijiuliza maswali mfululizo yaliyomfanya akose majibu.
“Sasa kwa nini haniitikii? Ina maana hajasikia? Na kile kishindo ni cha nini?” Mkuu wa chuo alijiuliza maswali mfululizo yaliyomfanya akose majibu.
Kitu pekee alichoona kinafaa kwa wakati huo, ilikuwa ni kwenda kugonga mlango wa bafuni kutaka kuhakikisha kama Karen ndiye aliyekuwa akioga.
Baada ya kugonga mara moja tu, alisikia sauti ya Karen kutoka ndani ya bafu akimwambia kwamba amsubiri kidogo kwa sababu alikuwa anaoga.
Baada ya kugonga mara moja tu, alisikia sauti ya Karen kutoka ndani ya bafu akimwambia kwamba amsubiri kidogo kwa sababu alikuwa anaoga.
“Ukimaliza kuoga nataka kuzungumza na wewe ofisini kwangu, usichelewe,” alisema mkuu wa chuo na kutoka kurudi ofisini kwake huku akiwa na mawazo mengi ndani ya kichwa chake. Hakika mwenendo wa Karen ulishaanza kumshtua hata yeye kwani maisha yake yalikuwa na mambo mengi sana yasiyoeleweka.
“Yaani muda wote wenzake wanaomboleza yeye yupo tu chumbani kwake, wala hana hata wasiwasi! Lazima kuna mambo atakuwa anayafahamu kuhusu hiki kinachoendelea,” alisema mkuu wa chuo wakati akiendelea kupiga hatua fupifupi kuelekea ofisini kwake, kichwa akiwa amekiinamisha.
***
Karen aliendelea kujimwagia maji ya baridi, huku akiwa ameuma meno yake kutokana na maumivu aliyokuwa anayahisi mwili mzima kutokana na purukushani aliyokutana nayo. Alibaki kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.

Alishangaa alipata wapi ujasiri na nguvu za kufanya tukio kubwa kama lile kisha kurudi chumbani kwake salama bila kugundulika na mtu yeyote. Aliendelea kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu, huku maji ya baridi yakiendelea kutiririka mwilini mwake.
“Nisamehe matron, siyo mimi! Hukuwahi kunifanyia jambo lolote baya kustahili kifo cha kikatili namna hii, hata sijui ni kitu gani kinachoendelea kwenye maisha yangu,” Karen alijisemea kimyakimya huku akishika rozali aliyokuwa ameivaa shingoni.
Kumbukumbu zote za jinsi alivyofanya tukio la kikatili, la kuyakatisha maisha ya matron wake kisha kwenda kuutupa mwili wake kwenye msitu mkubwa uliokuwa nyuma ya chuo hicho, zilianza kujirudia kwenye kichwa chake kama mkanda wa video.
Alikumbuka jinsi alivyojaribu kutoroka lakini akajikuta akirudishwa ndani ya chumba chake na kupewa kazi ya kuhakikisha anamuua matron wake kabla hajatoa siri ya alichokigundua kwenye chumba chake.
Alikumbuka jinsi alivyomfuata matron wake nyumanyuma mpaka ofisini kwake, jinsi alivyomkaba kwa nguvu na kusababisha purukushani kubwa chumbani kwake mpaka alipofanikiwa kumzidi nguvu na kuanza kumcharanga kwa kutumia kisu kikubwa.

Alikumbuka jinsi alivyofanya tukio hilo bila kuwa na hata cheembe ya wasiwasi, kisha akapasua kioo cha dirisha na kuuburuza mwili wa matron huyo mpaka nje, jinsi alivyoendelea kuuburuza bila kuonekana na mtu yeyote mpaka alipozamia kwenye msitu huo.
Alikumbuka pia jinsi alivyokurupushwa na polisi, akiwa amekaa pembeni ya mwili huo, akijiuliza kumetokea nini mpaka akawa na roho ya kikatili namna hiyo, jinsi alivyokoswakoswa na risasi kadhaa na hatimaye alivyorudi kimiujiza chumbani kwake na kujishtukia akianguka kwa nguvu sakafuni.
“Lakini mimi siyo mchawi na wala sijawahi kufikiria kuwa mchawi, inawezekanaje nifanye haya yote bila ridhaa yangu? Kwa nini sina nguvu za kukataa kufanya jambo nisilolitaka?” Karen aliendelea kujiuliza huku mkono wake mmoja ukiwa kwenye rozali yake.
Alizinduliwa kutoka kwenye dimbwi la mawazo baada ya kusikia mlango wa bafuni kwake ukigongwa tena.“Wee Karen unaoga mwaka mzima? Nimekwambia nataka kuzungumza na wewe sasa hivi, hebu toka huko bafuni,” Karen alimsikia mkuu wake wa chuo akizungumza kwa sauti kubwa, akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Ilibidi afunge bomba, akajifunga taulo na kuziacha nguo zake nyingine zilizokuwa zimelowa damu kulekule bafuni, akatoka huku akiwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wake kwani kwa jinsi mkuu wa chuo alivyokuja kishari, ilionesha lazima kuna jambo analifahamu kuhusu kilichotokea.
“Vaa nguo zako haraka, nataka tuongozane mpaka ofisini kwangu.”
“Sawa mkuu lakini naomba utoke kwanza nje nivae nguo.”
“Vaa nguo zako haraka, nataka tuongozane mpaka ofisini kwangu.”
“Sawa mkuu lakini naomba utoke kwanza nje nivae nguo.”
“Vaa hapahapa, kwani wewe si mwanamke kama mimi? Unaogopa nini?” mkuu wa chuo alisema lakini Karen hakuwa tayari kubadili nguo mbele ya mkuu huyo wa chuo kwani alijua siri yake aliyoificha kwa kipindi kirefu kuhusu jinsia yake, inaweza kufichuka.
Baada ya kuona amesimamia msimamo wake, ilibidi mkuu wa chuo atoke na kumuacha peke yake lakini akamwambia anamsubiri mlangoni. Alipotoka tu, harakaharaka Karen alibadilisha nguo na kuvaa joho la kitawa, akatoka na kuongozana na mkuu huyo wa chuo mpaka ofisini kwake.
“Karen!”
“Karen!”
“Abee!”
“Unajua kinachoendelea hapa chuoni?”
“Najua mkuu.”
“Unajua nini?”
“Unajua kinachoendelea hapa chuoni?”
“Najua mkuu.”
“Unajua nini?”
“Kwamba kuna muuaji kutoka ndani yetu aliyefanya mauaji ya watu wawili leo.”
“Muuaji kutoka ndani yetu? Umejuaje kuwa anatoka ndani yetu?”
“Nimewasikia polisi wakisema hivyo.”
“Muuaji kutoka ndani yetu? Umejuaje kuwa anatoka ndani yetu?”
“Nimewasikia polisi wakisema hivyo.”
“Wakati tukio la kwanza linatokea wewe ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa nimelala chumbani kwangu.”
“Kweli?”
“Ndiyo mkuu.”
“Nilikuwa nimelala chumbani kwangu.”
“Kweli?”
“Ndiyo mkuu.”
“Mbona kuna watu wanasema ulionekana nje usiku wa manane, muda mfupi kabla ya tukio?”
“Nilitoka mra moja tu lakini niliporudi sikutoka tena mpaka asubuhi.”
“Na kuhusu tukio la leo?”
“Nilitoka mra moja tu lakini niliporudi sikutoka tena mpaka asubuhi.”
“Na kuhusu tukio la leo?”
“Nilikuwa chumbani kwangu.”
“Mbona kuna watu ambao mara ya mwisho walikuona ukielekea ofisini kwa matron na baada ya hapo ndiyo tukio la pili likatokea?” mkuu wa chuo alikuwa akimhoji Karen huku amemkazia macho. Hakuonesha masihara hata kidogo. Karen akaanza kubabaika huku akijiumauma.

Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.

Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu.
Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumatatu kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda.
Je, nini kitafuatia? Usikose Jumatatu kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda.
Tags
Hadithi & Simulizi