MAMA: KANUMBA ALIKUWA WA KIPEKEE

Mama Kanumba akitoa shukrani kwa waliohudhuria Kanumba Day, Dar Live.

MAMA mzazi wa staa wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoha amesema anamkumbuka mwanaye kwa mengi kwa sababu alikuwa wa kipekee kwake.
Mama Kanumba wakati wa ibada ya kumbukumbu ya mwanaye.
Akizungumza na mwandishi wetu juzi, katika Makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  mama Kanumba alisema ana mengi ya kukumbuka kuhusu mwanaye.
Alisema: “Kanumba alikuwa na upendo sana. Si kwangu tu, hata kwa wengine aliohisi wana uhitaji. Hakuwa mchoyo, kwa kweli kila ninapomkumbuka naumia sana.
“Namkumbuka sana, ameondoka na upendo wake. Alikuwa ndiye mfariji wangu mkubwa. Nitajitahidi kuwasaidia wasiojiweza kila ninapopata nafasi ili kumuenzi.”
Alisema, katika kumuenzi mwanaye Kanumba, ndiyo maana kama familia wameanzisha mfuko wa Kanumba walioupa jina la Kanumba Foundation kwa lengo la kuwasaidia wahitaji.
Shughuli ya kumbukumbu ya marehemu Kanumba ilianzia kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Temboni kisha makaburini na baadaye usiku katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala – Zakhem, Dar.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post