UTUMWA WA MAPENZI NJE YA NDOA-17


ILIPOISHIA...
Kitu ambacho Vanessa hakukijua ni kwamba safari ile ilikuwa inaishia hotelini!
SASA ENDELEA.....
HAPAKUWA mbali sana, mwendo wa dakika tano tu kutoka barabara kuu ya kuelekea Chuo cha Ardhi, gari lilisimama mbele ya jengo kubwa, refu lililonakshiwa na vioo tupu. Bango kubwa juu ya jengo hilo lilisomeka; SAMSHAL HOTEL.
Hisia za Vanessa zilikuwa juu sana. Hakuzungumza kitu. Ni kama alikuwa akisubiria kuona kitakachotokea. Baada ya kuegesha tu, Ngoma alishuka haraka kisha akazunguka upande wa pili na kumfungulia Vanessa mlango.
Akashuka na kusimama kimya chini kama aliyekuwa akisubiria amri kutoka kwa Ngoma. Hakufanya makosa. Alimshika mkono na kumkokota kuelekea mapokezi. Alimuacha msichana aliyekuwa mapokezi na kuifuata lifti iliyokuwa mbele yao, akabonyeza kitufe kilichokuwa mlangoni, mlango ukafunguka.
Akamshika mkono na kumwingiza kwenye lifti.
Kidole gumba cha Ngoma kikabonyeza kitufe kilichokuwa kimeandikwa nambari nane. Lifti ikaanza kupaa. Hakuna aliyemzungumzisha mwenzake kabisa. Maandishi kwenye kioo pembeni ya mlango, yakaanza kuonyesha namba za ghorofa.
Ilipofika namba nane, ikasimama na mlango ukafunguka. Wakatoka na kuanza kutembea kwenye korido. Mlango wenye maandishi Mikumi – 6, ndipo waliposimama. Ngoma akatoa kadi mfukoni na kuielekeza mlangoni.Ukafunguka!Bado walikuwa mabubu! Waliingia kwenye sebule nzuri ya kisasa, iliyokuwa na kila kitu cha kifahari.
Ni kama walikuwa nyumbani. Pembeni ya sebule hiyo kulikuwa na sehemu ndogo iliyotengwa kwa ajili ya chakula. Friji kubwa na jiko dogo lililokuwa na majiko manne; mawili ya gesi na mengine ya umeme.
“Karibu, jisikie huru tafadhali.”
“Ahsante Ngoma, lakini hapa ni hotelini.”
“Najua...nilifanya hivyo kwa sababu nataka tuwe huru. Hakuna kibaya kitakachotokea, lakini nikuambie ukweli, nahisi mwili mzima unachemka... nasikia joto kali kuliko kawaida. Niruhusu nikajimwagie maji!”
“Mh! Ngoma jamani...mambo ya kuoga tena?” akasema Vanessa kwa sauti ile tamu ambayo kwa mumewe Harrison ilikuwa burudani tamu ajabu, leo hii Ngoma anaisikia.
Ngoma akazidi kuchanganyikiwa. Mshawasha wa huba ukampanda. Alitamani kumvamia Vanessa na kujiridhisha, lakini akavumilia.

Haraka ya nini?
“Eti naharakia nini? Si ameshaingia hotelini? Kuna nini tena? Hata iweje, hawezi kutoka salama hapa. Nitahakikisha anakuwa mikononi mwangu. Lazima niufurahie uzuri wake, lazima...” akajisemea moyoni mwake Ngoma.
“Hata kama ungekuwa wewe usingeweza kuvumilia joto kali kama hili linalonichoma mwilini mwangu. Naomba ruhusa yako mama.”
“Sawa.” Ngoma hakukawia, haraka akaingia chumbani ambapo bafu lilikuwa humo. Alitumia dakika saba tu, tayari alirudi sebuleni.
Alirudi akiwa tofauti na alivyoingia; sasa alikuwa amevalia taulo tu! Akazidi kumpa shida Vanessa.
Pamoja na kwamba aligundua kuwa Ngoma alikuwa mwanaume mtanashati, hakutegemea kama alikuwa na mwonekano mzuri wa kiwango kile. Ngoma alikuwa na mwonekano kamilifu wa kiume. Milima miwili iligawanyika juu ya kifua chake, ilimfanya kila aliyemwangalia asihoji kuhusu ufanyaji wa mazoezi wa Ngoma.
Alikuwa mwanaume wa shoka. Hakuwa na tumbo kubwa kama vijana wengi wa mjini, wapiga maji wanavyokuwa. Manyoya yaliyozagaa tumboni na kufunika kitovu chake, yalimwongezea Vanessa uchu.
“Sijui itakuwaje? Nawezaje kumsaliti mume wangu kirahisi namna hii? Hata kama angekuwa nani, hawezi kutoka salama hapa. 
Sijui kama nitatoka salama katika mazingira haya. Ngoma lazima atanipata leo!” aliwaza Vanessa.
Hata yeye alijishangaa kwa namna alivyopoteza msimamo kirahisi kiasi kile.Ngoma alimfuata Vanessa na kufanya kama anataka kumnong’oneza kitu sikioni. Lilikuwa kosa. Alichokifanya Ngoma ilikuwa ni kuutumbukiza ulimi wake wote sikioni mwa Vanessa kisha akaanza kuutembeza kwa ufundi wa hali ya juu.
Alihisi kama shoti ya umeme ikiingia mwilini mwake, fumba na kufumbua, tayari wote walikuwa watupu wakimaliza kila kitu kwenye sofa kubwa pale sebuleni. Ni kama walikuwa wamedhamiria kuonyeshana kazi.
Kila mmoja alionyesha ufundi wake wote. Wakati yote haya yakiendelea, Harrison alikuwa hajitambui - mgonjwa, tena yupo ICU – nje ya nchi, baada ya upasuaji uliochukua saa kadhaa chini ya jopo la madaktari bingwa wa mfumo wa utumbo mpana.
Siyo sawa!
***
 Macho ya Dk. Iyina yalitua tena kwenye chombo kinachosoma mapigo ya moyo na shinikizo la damu. Angalau sasa Harrison alionekana akiweza kupumua vizuri kiasi kwa msaada mdogo wa mashine ya oksijeni, mapigo ya moyo yakarudi taratibu kwenda kwenye hali ya kawaida.Shinikizo la damu liliendelea kushuka taratibu.
Lilikuwa juu lakini kwa hali aliyokuwa nayo awali, ni kama alikuwa katika hali ya kawaida. Kipimo kilisoma 140/90 mmHg. Hii ni kutoka 190/100 mmHg, hali ilikuwa mbaya sana kabla!
“Afadhali!” alisema kwa Kihindi Dk. Iyina.
Hali hiyo ilimfanya afikie uamuzi wa kuchomoa mpira wa oksijeni puani mwake. Harrison akaonekana kuhangaika kidogo. Akaurudisha haraka. Akaweka vizuri mkono wa Harrison uliokuwa na dripu, kisha akatabasamu!“Kijana mzuri sana huyu. Itakuwa furaha yangu kubwa sana kama akipona,” aliwaza Iyina.
Saa tatu baadaye, Harrison alizinduka. Alikuwa kama aliyepumbazwa.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post