Mambo yalianza kama masihara, baadaye yakaibuka machafuko makubwa ya kisiasa kati ya watu wa Jamhuri ya Wabara na Wapwani yaliyosababisha maafa makubwa kwa watu wasio na hatia. Katika machafuko hayo, Kalunde, msichana mdogo mrembo, anawapoteza wazazi wake wote wawili, ndugu zake wa tumbo moja na mchumba wake, Maguha waliokufa kwa kukatwakatwa mapanga.
Kifo cha Maguha, mwanaume aliyetokea kumpenda kwa moyo wake wote, ndicho kinachoonekana kumgusa zaidi. Kwa bahati nzuri, anafanikiwa kutoroka mapigano na kukimbilia Tangani akiwa na mtoto mdogo, Khalid. Wanafika salama baada ya kuokolewa baharini na meli ya wavuvi.
Wanapata matibabu na kuyaanza maisha mapya baada ya kupewa hifadhi na Kuruthum na mumewe, Mohamed ambaye ni mfanyabiashara mkubwa jijini Tangani.
Kiapo chake kwamba hatampenda mwanaume mwingine yeyote baada ya kifo cha Maguha, unaanza kuyumbayumba baada ya kukutana na kijana wa kichotara, Faheed ambaye anaonesha kitendo cha kishujaa mno kwa kuutoa sadaka uhai wake ili kuwaokoa Kalunde na Khalid wakati nyumba waliyokuwa wakiishi ikiungua vibaya, wao wakiwa wamenasa ndani.
Licha ya kufanikiwa kuwaokoa, yeye anakwama na kuungua vibaya na moto mkali na sasa yupo kwenye hatua za mwisho za kupigania uhai wake. Bila kujua kilichompata Faheed, Kalunde anajikuta akianza kumpenda kijana huyo na sasa anawasumbua Kuruthum na mumewe akitaka Faheed aletwe kuwaona hospitalini hapo.Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…“
Mbona sikuelewi mama? Kwa nini unalia?” Kalunde alihoji, ikabidi Mohamed aingilie kati na kumsaidia mkewe kumuweka sawa Kalunde lakini bado maelezo yake hayakutosha kumtuliza Kalunde. Tayari alishahisi kwamba kuna jambo halipo sawa ila Kuruthum na mumewe wanamficha.
“Niambieni ukweli, Faheed yupo wapi? Na kwa nini mnalia?”
“Niambieni ukweli, Faheed yupo wapi? Na kwa nini mnalia?”
“Kalunde, tulia kwanza utibiwe mpaka utakapopata nafuu, hayo mambo mengine utayajua tu.”
“Hapana sitaki, kamleteni Faheed la sivyo mniambie nini kilichompata,” Kalunde alizidi kuwa mbogo, akawa anatishia kujichomoa dripu aliyochomekwa kwenye mshipa wake wa mkono endapo hataambiwa ukweli.
“Hapana sitaki, kamleteni Faheed la sivyo mniambie nini kilichompata,” Kalunde alizidi kuwa mbogo, akawa anatishia kujichomoa dripu aliyochomekwa kwenye mshipa wake wa mkono endapo hataambiwa ukweli.
Ilibidi Kuruthum na mumewe watoke nje kujadiliana kwanza kwani hakuna aliyekuwa na majibu juu ya nini kifanyike.
“Mke wangu, mi nafikiri tumwambie tu, hakuna haja ya kuendelea kumficha.”
“Hapana mume wangu, si unaona hiyo hali yake ilivyo? Tunaweza kumsababishia madhara zaidi, tumuache mpaka atakapopona ataujua mwenyewe ukweli.”

“Hapana, ni haki yake kujua kwa sababu huo ndiyo ukweli, hata akiumia sisi tutakuwa tumeutua mzigo.”
“Jamani mume wangu, unafikiri atalipokeaje suala hilo?”
“Jamani mume wangu, unafikiri atalipokeaje suala hilo?”
“Hatuna cha kufanya Kuruthum mke wangu, mimi naenda kumwambia,” Mohamed alisema huku akigeuka na kutaka kurudi wodini lakini mkewe alimshika mkono na kumrudisha.
“Basi sawa utaenda kumwambia lakini naomba ufanye kitu kimoja kwanza. Tuwapigie simu wazazi wa Faheed ili tujue hali ya mgonjwa inaendeleaje kwanza kisha tuwaombe idhini ya kumwambia Kalunde juu ya kilichompata kijana wao.”

“Hilo la kuwaomba idhini wala siyo la msingi labda kumjulia hali mgonjwa ndiyo kubwa,” alisema Mohamed huku akitoa simu yake ya kisasa na kubonyeza namba za simu za baba yake Faheed alizokuwa akizitumia nchini Afrika Kusini.
Baada ya muda, tayari alikuwa hewani akizungumza na baba yake Faheed ambaye alikuwa akiongea kwa uchungu wa hali ya juu. Akawataarifu kwamba hali ya mgonjwa bado haitii matumaini hata kidogo hivyo ni bora waendelee kumuombea kwa Mungu ayanusuru maisha yake.
Baada ya kumaliza kuzungumza na simu, Mohamed alikata na kumgeukia mkewe ambaye muda wote alikuwa makini kusikiliza mazungumzo kati ya mumewe na baba Faheed.
“Anasemaje?”
“Anasemaje?”
“Bado hali ya Faheed ni mbaya sana, anasema haitii matumaini hata kidogo,” alisema Mohamed na kushusha pumzi ndefu. Wote wakakubaliana kwamba ni bora wakamwambie Kalunde ukweli kwani chochote kinaweza kutokea muda wowote.
“Nataka mniambie ukweli, la sivyo sitakula wala kunywa dawa, ni bora nife tu,” Kalunde alisema huku akianza kuangua kilio, Kuruthum na mumewe wakamtuliza na kumwambia kuwa wapo tayari kumueleza kilichotokea. Akanyamaza huku akishusha pumzi ndefu, akatega masikio kwa makini.
“Unakumbuka siku ya ajali ilivyokuwa?”
“Unakumbuka siku ya ajali ilivyokuwa?”
“Nakumbuka baadhi ya vitu, vingine sivikumbuki.”
“Enhee! Wakati moto unawaka, Faheed alikuja nyumbani kwetu na kukuta nyumba inawaka moto kwa kasi, akajaribu kuingia lakini askari wa kikosi cha zimamoto wakamzuia kwani hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba kama angeingia, uwezekano wa kutoka ulikuwa mdogo sana.”

“Ikawaje?” Kalunde alihoji huku akijiweka vizuri pale kitandani, macho ya shauku yakiwa yamemtoka.
“Alipoona njia zote zimeshindikana na moto unazidi kuwaka, ilibidi atumie ujanja, akampiga askari mmoja na kuvaa mavazi yake ya kuzuia moto kisha akajitosa katikati ya moto mkubwa mpaka ghorofani mlikokuwa wewe na Khalid.”

“Mungu wangu, nini kikafuatia?”
“Tunamshukuru sana Faheed kwani alifanikiwa kuingia mpaka kwenye chumba mlichokuwa wewe na Khalid, akawaokoa na kuwarusha nje mpaka kwenye ‘swimming pool’ ambako mliokolewa na kukimbizwa hospitalini.”
“Na yeye je, nini kilifuatia?”

“Ni bahati mbaya sana, yaani hata sijui nikueleze vipi.”
“Whaaat? Hebu niambie ukweli, nini kilimpata?” Kalunde alipaza sauti, Mohamed akameza funda la mate na kumgeukia mkewe ambaye naye alikuwa amejiinamia, akampa ishara ya kuendelea kumueleza Kalunde kila kitu.

“Alijitahidi kwa kadiri ya uwezo wake lakini kwa bahati mbaya, alishindwa kutoka kwenye moto. Nguo alizokuwa amevaa zikashindwa kumkinga asiungue, inasikitisha sana lakini ndiyo hivyo imeshatokea inabidi tuendelee kumuombea kwa Mungu.”
“Mbona sikuelewi baba? Kwa hiyo Faheed alikufa au yupo hai?”
“Kalunde Faheed hakufa ila kama nilivyokueleza, aliungua vibaya sana. Mpaka askari wa kikosi cha zimamoto wanaenda kumtoa, alikuwa ameungua karibu mwili mzima, akakimbizwa mpaka hapa hospitalini lakini hali yake ikazidi kuwa mbaya.”

“Kwani hivi sasa yuko wapi? Nipelekeni nikamuone hata kama ana hali mbaya maana najua haya yote yametokea kwa sababu ya upendo wa dhati aliokuwa nao kwangu na mwanangu Khalid,” alisema Kalunde huku akilia kwa uchungu.
Mohamed akamueleza wazi kwamba kutokana na hali aliyokuwa nayo, ilibidi wazazi wake wamkodie ndege maalum iliyomsafirisha mpaka Hospitali ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini ambako ndiko anakoendelea kutibiwa mpaka wakati huo.
“Eeeh Mungu wa Yakobo, naomba onesha muujiza wako Faheed apone,” alisema Kalunde huku akiendelea kulia kwa uchungu. Akawaomba Mohamed na mkewe Kuruthum kama kuna uwezo, wampeleke nchini Afrika Kusini japo akamuone tu roho yake itatulia.
“Haiwezekani Kalunde, wewe mwenyewe hali yako bado haijawa nzuri, cha msingi ni kuendelea kumuombea kwa Mungu atapona,” alisema Kuruthum huku akiwa amekumbatiana na mumewe, wakawa wanamshuhudia jinsi Kalunde alivyokuwa analia kwa uchungu. Kazi ikabadilika ambapo wote wawili walianza kumbembeleza msichana huyo akubaliane na kilichotokea.
“Cha msingi ni kumshukuru Mungu kwa miujiza aliyotufanyia, bila Faheed sijui kama mngekuwa hai mpaka muda huu,” alisema Kuruthum, Kalunde akawa anatingisha kichwa kama ishara ya kukubaliana na alichokuwa anaambiwa huku akiendelea kulia kwa uchungu.
Tags
Hadithi & Simulizi