KALUNDE ameamua kutoroka kuelekea Bara ndani ya mtumbwi akiwepo mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Rahim pamoja na mtoto mdogo aliyekabidhiwa na mwanamke aliyekuwa akifa. Ni safari ndefu na hakuna kati yao anayejua kama watafika waendako.
Ghafla anamshuhudia Rahim akianguka na kufa, anamlaza pembeni na safari kuendelea. lakini siku mbili tena baadaye mtoto mdogo naye anatulia kimya ishara kwamba tayari amekata roho.
Kalunde analia kwa uchungu, lakini anapiga moyo konde na kuendelea na safari ndani ya mtumbwi akiwa na maiti za watu wawili.Siku ya tatu macho yake yanaona giza nguvu zinamwishia hapo ndipo anaamini kwamba naye pia mwisho wake umefika, akalalakatikati ya maiti ya mtoto na Rahim.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...
Ukimya mkubwa ulitawala, mvua kubwa ikiendelea kunyesha na upepo mkali kuvuma. Ingawa mtumbwi haukuwa na mpiga kasia, ulizidi kupelekwa taratibu na maji huku mizigo ya watu watatu, watu wazima wawili na mtoto mmoja ikiwa ndani yake.
Giza lilizidi kuongezeka machoni mwa Kalunde, kama vile ambavyo mtu hupunguza mwanga wa chemli akielekea kuizima, hatimaye kukawa hakuna mwanga tena na fahamu zikamwondoka Kalunde, hakuelewa tena kilichoendelea.
Mwanga uliporejea machoni ulikuwa mkali na katikati ya mwanga huo alimwona Maguha akiwa amepanua mikono yake yote miwili na kumkaribisha, huku akisema “Come baby, we can get married here!” maneno ya kiingereza yaliyomaanisha “Njoo mpenzi, tunaweza tukaoana hapa!” Moyo wa Kalunde ukashtuka, lakini wakati akiendelea kushangaa, aliwaona baba, mama na ndugu zake wakiwa wamevalia mavazi ya rangi nyeupe, wote wakiwa wametanua mikono yao na kumkaribisha mahali ambako hakupafahamu nyuso zao zikiwa zimefunikwa na tabasamu.
“Tumekusubiri kwa muda mrefu!” ilikuwa ni sauti ya mama yake.
“Njoo mwanangu, tuishughulikie sasa harusi yako na Maguha.”
“Hapana baba! Siwezi kuja, nataka kwenda kumchukua mtoto wangu!”
“Mtoto wako?”
“Ndiyo.”
“Njoo mwanangu, tuishughulikie sasa harusi yako na Maguha.”
“Hapana baba! Siwezi kuja, nataka kwenda kumchukua mtoto wangu!”
“Mtoto wako?”
“Ndiyo.”
“Una mtoto?”
“Ndiyo.”
“Umezaa?”
“Ndiyo.”
“Na nani?”
“Ndiyo.”
“Umezaa?”
“Ndiyo.”
“Na nani?”
Kalunde hakujibu swali hilo badala yake aligeuka na kukimbilia upande wa pili, ambako mtoto mdogo aliyekabidhiwa na mwanamke aliyekuwa akifa alikuwa mikononi mwa aliyeonakana kama binadamu lakini mwenye mabawa, hakuwa na mtoto huyo tu, bali pia Rahim alikuwa begani kwake! Wote alikuwa akitokomea nao kwenda upande wa pili kulikokuwa na giza.
Kalunde alipomfikia kiumbe huyo aliyafanana kabisa sura na malaika aliozoea kuwaona kwenye vitabu vya dini, alisimama mbele yake na kumshika mtoto miguu, hapo hapo akaanza kumvuta kwa nguvu kubwa mpaka akafanikiwa kumwondoa mikononi mwa malaika huyo.
***
“Huyu ameshakufa tayari, ila huyu mtoto na huyu binti bado wako hai, presha na joto lao la mwili liko chini sana, lazima tuvipandishe kwa joto, wapelekeni kwenye chumba ambacho huwa tunalaza watoto njiti, joto la kule litasaidia, kwa kupandisha presha wawekewe dripu za Normal Saline haraka iwezekanavyo!”

“Sawa daktari, huu ni muujiza, walivyokuwa wakionekana ni kama vile walikuwa wamekufa kabisa!”
“Hata mimi nashangaa, nimefanya kazi hospitali kwa miaka ishirini na tano lakini sijawahi kuona wagonjwa waliokuwa na hali mbaya kama huyu dada na mtoto halafu ghafla tu, mapigo yao yakakaa sawa.”
“Hata mimi nashangaa, nimefanya kazi hospitali kwa miaka ishirini na tano lakini sijawahi kuona wagonjwa waliokuwa na hali mbaya kama huyu dada na mtoto halafu ghafla tu, mapigo yao yakakaa sawa.”
“Unaitwa nani?” Daktari alimuuliza mgonjwa.
“Kalunde.”
“Kalunde nani?”
“Kalunde Abdallah!”
“Unajua hapa uko wapi?”
“Hapana.”
“Kalunde.”
“Kalunde nani?”
“Kalunde Abdallah!”
“Unajua hapa uko wapi?”
“Hapana.”
“Mara ya mwisho unakumbuka ulikuwa wapi?”
“Baharini.”
“Na nani?”
“Rahim pamoja na mtoto wangu.”
“Ukitokea wapi?”
“Kisiwa cha Pwani, tulikuwa tukikimbia mauaji!”
“Mshukuru sana Mungu wako.”
“Baharini.”
“Na nani?”
“Rahim pamoja na mtoto wangu.”
“Ukitokea wapi?”
“Kisiwa cha Pwani, tulikuwa tukikimbia mauaji!”
“Mshukuru sana Mungu wako.”
“Mtoto wangu yuko wapi?”
“Huyo hapo kando ya kitanda chako.”
Kalunde alipojaribu kunyanyuka ili amwone mtoto, alishindwa, mwili wake haukuwa na nguvu za kutosha. Hata hivyo akamshukuru Mungu kujikuta yuko hai kwenye eneo ambalo hakulifahamu, alichokuwa akifahamu yeye wakati anapoteza fahamu ni kwamba kifo ndiyo kilikuwa mbele yake, sasa iweje awe hai? Hakuwa na jibu.

Alipofikishwa kwenye chumba cha kulaza watoto njiti, kilichokuwa na joto kubwa, alitundikiwa dripu kama daktari alivyoelekeza, vivyo hivyo ndivyo ilivyotendeka kwa mtoto, hali zao zikaanza kuimarika. Siku mbili baadaye Kalunde alikuwa na nguvu kabisa.
“Nani alituokoa?” alimuuliza muuguzi.
“Meli ya wavuvi.”
“Ilikuwaje?”
“Walipita wakaona mtumbwi usiku, waliposogea karibu waligundua ndani ya mtumbwi huo kulikuwa na binadamu wamelala, walichofanya ni kuingia ndani ya mtumbwi na kuwatoa, mlikuwa hamjitambui kabisa, mlipofikishwa hapa na kupimwa, daktari aligundua kuwa mmoja wenu ndiye alikwishakufa.”

“Masikini, ni Rahim huyo.” Aliongea Kalunde na kuanza kujifuta machozi.
“Hatujui anaitwa nani?”
“Naomba kumwona mtoto wangu!”
“Hivi ni mtoto wako wa kuzaa?”
“Ndiyo.”
“Hatujui anaitwa nani?”
“Naomba kumwona mtoto wangu!”
“Hivi ni mtoto wako wa kuzaa?”
“Ndiyo.”
“Mbona huonekani kama umezaa?”
“Nimezaa dada, mengine ni maumbile tu.”
“Anaitwa nani mwanao?”
“Khalid!”
“Mzuri.”
“Nimezaa dada, mengine ni maumbile tu.”
“Anaitwa nani mwanao?”
“Khalid!”
“Mzuri.”
“Ahsante, lakini hapa nilipo ni wapi?”
“Ni Tangani.”
“Ndiko mimi na Rahim, pamoja na mtoto wangu tulikokuwa tukielekea kabla Rahim hajaanguka na kufa.”
Mtoto akabebwa na kupelekwa kitandani kwake, afya yake ilisharejea kwenye hali ya kawaida kabisa kiasi cha kumfanya Kalunde asiamini muujiza uliokuwa umetokea.

Alipokumbuka taswira ya mama na mtoto huyo, wakati akimkabidhi mtoto na baadaye kufa, Kalunde alimshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea na aliahidi moyoni mwake kwamba angemtunza mtoto huyo hadi mwisho wa uhai wake.
“Nitatimiza wajibu wangu, nitakachokula utakula, nitakapolala utalala na nitakuwa tayari kufanya lolote kukulinda, wewe ndiye utakuwa mtoto wangu wa kwanza!” Kalunde aliwaza machozi yakimbubujika.
Baadaye alitafakari alichokiona kabla hajarejewa na fahamu zake, sura ya Maguha, wazazi na ndugu zake na kule walikokuwa, akaamini kabisa alichokiona ni taswira ya Mbinguni ambako walikuwa kwa wakati huo. Moyoni akaamini kama isingekuwa kwa kumrudia mtoto wake ambaye alimwondoa mikononi mwa malaika wa mauti, hata yeye kwa wakati huo angekuwa mbinguni na Maguha pamoja na familia yake.
Akaendelea kulia kwa muda mrefu kila alipoyafikiria maisha yake, alipotoka, alipokuwa na alikokuwa akielekea. Hakuona namna ambavyo angeweza kuishi bila familia yake, tumaini lote akalielekeza kwa Mungu. Hakika hakuwa na mtu yeyote aliyemfahamu katika katika nchi ya Bara.
Ni kweli babu zake walitokea huko miaka mingi kabla ya kwenda kuanzisha maisha visiwani Pwani, ambako mwanzoni walifanya kazi kwenye mashamba ya waarabu kama Watumwa, wakiitwa Wanyamwezi, lakini baadaye utumwa ulipopigwa marufuku walianza kuishi kawaida, kama ilivyokuwa kwa wakazi wengine wa Kisiwa hicho.
“Mizizi yangu iko hapa Bara, lakini simfahamu mtu yeyote!” alimwambia muuguzi aliyekuwa jirani yake.
“Kwa hiyo huna ndugu hapa Tangani?”
“Kwa hiyo huna ndugu hapa Tangani?”
“Kabisa, sikuwahi kufika huku, nilizaliwa Kisiwa cha Pwani, nikasomea na kukulia huko.”
“Sasa utafanyaje na kesho wanafikiria kukuaga?”
“Yaani sijui, Mungu atanionyesha pa kwenda!”
“Anasema si mwenyeji hapa Tangani?” mama mmoja Chotara wa Kiarabu aliyekuwa amelazwa kitanda cha jirani alimuuliza muuguzi.

“Binti, huna ndugu hapa?”
“Sina ndugu mama.”
“Pole sana!”
“Ahsante.”
“Sina ndugu mama.”
“Pole sana!”
“Ahsante.”
“Basi nikiagwa hiyo kesho tutaondoka sote hadi nyumbani kwangu, utaishi na sisi mpaka utakapojipanga!”
“Alhamdulillah!”
Kalunde akaamini kweli Mungu alikuwa pamoja naye, siku iliyofuata wote pamoja na mwanamke huyo aliyeitwa Kuruthum Mohamed waliruhusiwa na kupanda gari ya familia hadi nyumbani kwa mama huyo, Kalunde alishangazwa na utajiri wa nyumba aliyoingia.

Ilikuwa ni nyumba ya ghorofa mbili, waliyoishi familia mbili za mtu na kaka yake, wote walikuwa ni ndugu na walifanya biashara pamoja, Kalunde alitambulishwa kwa familia nzima na kila mtu alimfurahia yeye na mtoto wake, jioni ya siku hiyo aliwasimulia historia yake ya maisha na yaliyomtokea mpaka akajikuta Tangani, kila mtu alimwaga machozi.
“Utakaa na sisi kama mtoto wa nyumbani, wala usifikirie kabisa yaliyotokea nyuma, Mungu amekuweka mikononi mwetu kwa sababu maalum, tutatimiza wajibu wetu kama wewe ulivyotimiza kwa mtoto wako Khalid!””
“Ahsanteni.”
“Ahsanteni.”
Ukawa mwanzo wa maisha mapya kwa Kalunde, lakini hata siku moja hakumsahau Maguha na wazazi wake, aliwaombea kila siku na alisikitishwa na mauaji yaliyokuwa yakiendelea kisiwani Pwani.
Tags
Hadithi & Simulizi