Kila siku matukio ya kusikitisha ndiyo yanayotawala maisha yake, likiisha tatizo moja linaanza jingine. Msichana mdogo Amelia anateseka kwa kipindi kirefu na aliwahi kupata raha kiduchu kabla wazazi wake hawajafariki.
Baada ya vifo vya wazazi wake, maisha yake yanaharibika kabisa, kila siku ni shida, matatizo na majonzi. Anateseka kwa kipindi kirefu, maisha yake yakiwa yamezingirwa na giza nene.
Baada ya vifo vya wazazi wake, maisha yake yanaharibika kabisa, kila siku ni shida, matatizo na majonzi. Anateseka kwa kipindi kirefu, maisha yake yakiwa yamezingirwa na giza nene.
Yupo kwenye Hospitali ya Apollo, Mumbai nchini India ambako mtoto ambaye kwa kipindi kirefu alikuwa akiamini ni wa kwake, anasumbuliwa na tatizo la kuvimba kichwa au kitaalamu Hydrocephalus na sasa zimebakia saa chache tu kabla hajafanyiwa upasuaji.
Hata hivyo, hali ya mtoto huyo inabadilika ghafla na licha ya madaktari wa hospitali hiyo kubwa inayotambulika dunia nzima kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao, mtoto huyo anapoteza maisha na kuzua simanzi kubwa kwa Amelia na Aristides.
Mwili wa marehemu unasafirishwa kutoka India mpaka Dar es Salaam lakini katika hali ya kushangaza, tangu Aristides na Amelia wawasili Uwanja wa Ndege na mwili wa marehemu, Esterlina hakuwepo nyumbani na hakuna aliyekuwa anajua chochote kuhusu mahali alipo.
Taratibu za msiba zinaandaliwa, watu wanakusanyika nyumbani kwa Aristides na maombolezo yanaendelea lakini bado hakuna anayejua mahali alipo mke wa Aristides. Kesho yake wanaenda kumzika mtoto huyo bila mama yake kuwepo. Tully anaamua kumfuata shoga yake nyumbani kwa mganga, Mlingotini, Bagamoyo.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…
“
Jamani nipo chini ya miguu yenu, nawaomba chondechonde, nyumbani kwake kuna matatizo makubwa. Amefiwa na mwanaye na wala hajui, nitawapa chochote mnachotaka,” Tulimwaga ‘Tully’ alikuwa akiwabembeleza wasaidizi wa mganga Kahungo kiasi cha kuanza kulengwalengwa na machozi.

Alipoona wasaidizi hao wa mganga wanakuwa wagumu kumuelewa, aliamua kutumia ushawishi wa fedha, akafungua pochi yake ndogo na kutoa noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi, wakatazamana na kutabasamu.
“Tusubiri tukajaribu ingawa tunajua tutamuudhi sana mzee na huenda akatuadhibu,” alisema mmoja kati ya wale wasaidizi, akaingia ndani na kutoa baiskeli, wakapakizana na safari ya kuelekea kwenye Msitu wa Gamutu kumfuata mganga Kahungo ikaanza.

Huku nyuma, Tully aliendelea kubabaika mithili ya kuku anayetaka kuatamia, moyoni alikuwa anamuomba Mungu wake Esterlina apatikane mapema kwani aibu iliyokuwa mbele yao ilikuwa ya karne.
Hakuweza kutulia sehemu moja, muda wote akawa anazungukazunguka eneo lote la nyumba ya mganga huku akijilaumu mno kwa hatua yake ya kumpeleka Esterlina kwa mganga.
Hakuweza kutulia sehemu moja, muda wote akawa anazungukazunguka eneo lote la nyumba ya mganga huku akijilaumu mno kwa hatua yake ya kumpeleka Esterlina kwa mganga.
“Ningejua wala nisingekubali kumleta, angalia yaliyotokea, eeh Mungu, onesha miujiza yako,” alisema Tully huku akiwa amejishika kichwani, uso wake ukiwa umebadilika rangi na kuwa mwekundu.
***
“Hii dawa utamchanganyia mumeo kwenye maji ya kuoga kwa muda wa siku saba, hii nyingine utamchanganyia kwenye kinywaji anachokipenda kama juisi, chai au uji kila siku kwa muda wa siku saba.
“Hii dawa utamchanganyia mumeo kwenye maji ya kuoga kwa muda wa siku saba, hii nyingine utamchanganyia kwenye kinywaji anachokipenda kama juisi, chai au uji kila siku kwa muda wa siku saba.
“Hizi nyingine utakuwa ukifukiza chumbani kwenu kabla ya kulala kwa kuchanganya na udi wa Uarabuni, nayo kwa siku saba. Kuhusu huyo kidudu mtu anayetaka kuivuruga ndoa yako, kazi yake itafanyika endapo ukileta nguo yake ya ndani, kipande cha sanda na maji ya kuoshea maiti, ukiipata tu basi umemaliza kila kitu.
“Halafu hakikisha kwamba unapobeba hizi dawa kurudi nyumbani, hupiti sehemu yenye makaburi wala kuyasogelea, hakikisha unazingatia masharti,” alisema mganga Kahungo baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya tambiko hilo, wakakubaliana wapumzike kidogo kabla ya kuanza tena awamu ya pili na ya mwisho.
“Sasa maji ya kuoshea maiti nitayapata wapi? Na hiyo sanda je?”
“Sasa maji ya kuoshea maiti nitayapata wapi? Na hiyo sanda je?”
“Kama unadhani huwezi kuleta, basi itabidi uniachie pesa kiasi nitakusaidia kutafuta, lakini nguo ya ndani ya huyo mbaya wako lazima uilete. Tena nilitaka kusahau, hakikisha haunyeshewi na mvua ukiwa umebeba dawa, umenielewa?” mganga alimuuliza Tully baada ya kumpa maelekezo.
Kabla Esterlina hajajibu, walishtushwa na ujio wa watu wawili waliokuwa wamepakizana kwenye baiskeli. Mganga akamtoa wasiwasi Esterlina baada ya kugundua kuwa walikuwa ni wasaidizi wake.
Akasimama huku akionesha kuwa na jazba kwani alishawakataza kumfuata pindi anapokuwa kwenye kazi ya matambiko. Nao kwa kujua kuwa walikuwa wamemkosea bosi wao, walishuka kwenye baiskeli harakaharaka na kumsogelea bosi wao kisha kumbusu miguuni, wakampa taarifa walizopewa na Tully.
“Kwa hiyo itakuwaje?”
“Kwa hiyo itakuwaje?”
“Amesema anaomba sana tumrudishe haraka ili awahi msiba wa mwanaye,” alisema msaidizi mmoja wa mganga, wote watatu wakageuka na kumtazama Esterlina ambaye hakuwa na taarifa juu ya chochote kilichokuwa kimetokea. Wakakubaliana kutomwambia chochote kwanza.
“Mama itabidi uondoke na huyu kijana wangu mpaka nyumbani, dawa tutamalizia baadaye,” alisema mganga akimwambia Esterlina, jambo ambalo lilimshangaza sana kwani hayo hayakuwa makubaliano yao. Hata hivyo, hakutaka kubisha, akakusanya kila kilichokuwa chake pamoja na dawa alizopewa, akapakizwa kwenye baiskeli na msaidizi mmoja wa mganga akaanza kupiga peda kwa kasi kurudi nyumbani.
Baada ya karibu nusu saa, tayari walikuwa wamewasili nyumbani kwa mganga, Esterlina akapigwa na butwaa baada ya kufika na kuliona gari lake kwa mbali. Akawa anajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
“Tully, vipi kuna usalama kweli?” alisema Esterlina huku akiruka kutoka kwenye baiskeli aliyokuwa amepanda na kumkimbilia shoga yake huyo ambaye naye alipomuona, alimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu huku akilia.
“Inabidi tuondoke Esterlina, tena haraka iwezekanavyo.”

“Tuondoke? Kwani kuna nini mbona sikuelewi? Halafu nini kinachokuliza?”
“Utaenda kujua mbele ya safari, ingia kwenye gari tuondoke.”
“Lakini sijamaliza bado kufanyiwa dawa.”
“Utaenda kujua mbele ya safari, ingia kwenye gari tuondoke.”
“Lakini sijamaliza bado kufanyiwa dawa.”
“Nimekwambia tuondoke, kuna mazito yametokea,” alisema Tully akiwa tayari ameshafungua mlango wa gari, akaingia na kuliwasha na kumuacha Esterlina akiwa bado amepigwa na butwaa.
“Dada ungemsikiliza mwenzako, inawezekana kuna jambo zito limetokea, tutakuagia kwa mganga utakuja kumalizia dawa hata kesho,” alisema yule msaidizi wa mganga, Esterlina akawa hana ujanja zaidi ya kukubali kupanda kwenye gari na dawa zake.
Tully akaondoa gari kwa kasi kubwa na kuanza kuchanja mbuga kuitafuta barabara ya lami. Bado Esterlina aliendelea kumbana shoga yake amueleze kilichotokea lakini hakuwa mwepesi zaidi ya kuendelea kutokwa na machozi huku akizidi kukanyaga mafuta na kusababisha gari liende kwa kasi kubwa.
Waliingia kwenye barabara ya lami ambako Tully aliendelea kukimbiza gari kwa kasi kubwa utafikiri majambazi waliotoka kufanya tukio la uhalifu mahali. Ndani ya muda usiozidi saa moja, tayari walikuwa wameshawasili jijini Dar, Tully akaendesha gari moja kwa moja mpaka nyumbani kwa shoga yake huyo.
“Mungu wangu! Kuna nini tena?”
“Mungu wangu! Kuna nini tena?”
“Kuna msiba Esterlina, sikutaka kukwambia tangu awali. Mwanao amefia India tangu jana, mumeo amekuja na maiti,” alisema Tully, kauli iliyomfanya Esterlina asiyaamini masikio yake. Kweli kulikuwa na maturubai nje ya nyumba yao na kulikuwa na watu wenye nyuso za huzuni.
Kibaya zaidi, waliambiwa kuwa tayari maiti imeshapelekwa makaburini, tayari kwa kuzikwa. Ilibidi Tully awashe tena gari huku Esterlina akiangua kilio kilichowashangaza watu wengi.
Dakika chache baadaye, tayari walishafika makaburini, Esterlina akashuka haraka kwenye gari huku akipiga kelele kwa nguvu zilizowashtua waombolezaji waliokuwa kwenye hatua za mwisho za mazishi. Hakukumbuka tena masharti ya mganga wake.
***
Nisingependa kumaliza hadithi hii ya leo bila kukumbusha jambo muhimu la kutoa maisha yako kwa Mungu. Maisha tuliyonayo hapa duniani ni mafupi sana, yanapita kama maua yachanuavyo na kunyauka. Wengi unaowafahamu wamekufa lakini wewe unapumua, ni vyema basi kufikiria maisha baada ya kifo.

Kila siku jiulize: “Hivi nikifa leo nitakwenda jehanam au peponi?” Kila mmoja wetu analo jibu lake, bila shaka sote tungependa kwenda peponi. Kama hivyo ndivyo, basi tiketi ya kwenda huko ni matendo mema na kujiepusha na uovu. Tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele.
Je, nini kitafuatia? Usikose Alhamisi ijayo katika Gazeti la Amani
Tags
Hadithi & Simulizi