MELANIA (Kamanda Jenette) aliyekuwa kiongozi wa waasi Congolese Patriotic Front baada ya mumewe kufariki, anaamua kutoroka baada ya kuonana na mama yake mzazi aliyetaka kumuua bila kujua. Anafanikiwa kuwatoroka waasi wenzake lakini anakumbana na upinzani mzito toka kwa wenzake ambao walimuona ni msaliti hivyo hawakuwa tayari kuona akitoroka. Waliapa kumsaka kila kona kuhakikisha kabla hajavuka porini wanamuua.
Mbeba magogo porini aliwaokota wakiwa nusu wafu na kuwachukua ili awapeleke hospitali iliyopo Mji wa Bondo uliopo mpakani mwa nchi ya Kidemokrasi ya Congo na Afrika ya Kati. Lakini kabla hawajafika mbali wanapata taarifa toka wa mfanyakazi aliyemuacha kwenye mradi wa magogo kuwa jeshi la waasi wamewateka na kuchukua moja ya magari yao na kuwafuatilia ili wawaue wale wanajeshi wa kike waliowaokota porini.
Dereva anajitahidi kukimbiza gari ili kuwakimbia waasi kwa kuamini hata wao maisha yao yatakuwa mashakani. Lakini safari inaandamwa na mikosi kabla ya kufika Mji wa Bondo gari linavamiwa na askari waliotokea msituni na kuwaweka chini ya ulinzi kutaka kujua kwenye gari wameweka nini.
Dereva anawadanganya hakuna kitu zaidi ya magogo. Je, wale wanajeshi watakubaliana na dereva na kuliacha gari lipite? Ili kujua yote
SONGA NAYO…
WALI la mwanajeshi aliyekuwa amelisogelea lori la magogo lilimfanya dereva ababaike.
“Ndi…ndi…yo.”
“Mbona kama unababaika?”
“Ha…pana nipo sawa.”
“Mutombo hebu panda juu ukague amebeba nini huenda wameficha wanajeshi,” alisema kiongozi wao.
Mwanajeshi aliyekuwa ameshikilia SMG aliining’iniza bunduki yake begani na kupanda juu huku wengine bunduki zao zikielekezwa kwenye gari. Mwenye gari aliomba Mungu watu aliowachukua wasionekane japo ilikuwa ni vigumu kutoonekana.
Baada ya Mutombo kupanda juu alisema kwa sauti ya juu. Alianza kukagua lakini alishtuka kuona magwanda ya jeshi la waasi. Alitoa bunduki yake begani na kuishika mkononi. Aliwaelekezea mtutu wa bunduki na kuwaweka chini ya ulinzi. Lakini alishangaa kuona watu wenyewe hawageuki, alipowachunguza aligundua wamepoteza fahamu. Alimuuliza dereva kwa sauti ya juu.
“We mbwa! Hawa kinanani?”
“Umeona nini?” aliuliza kiongozi wake.
“Kuna mwanajeshi wa waasi wamemficha kwenye magogo.”
“Jamani sijawaficha nimemuokota porini nampeleka hospitali.”
“Unatuchezea akili shukeni chini,” ilitolewa amri.
Dereva na msaidizi wake waliteremka chini na kuamliwa kupiga magoti na kunyoosha mikono juu.
“Sisi tunakesha porini kuwatafuta waasi kumbe kuna watu wanatuhujumu,” alisema askari mmoja aliyekuwa amenyoa kiduku.
“Jamani mi ni mtu mwema kabisa, siwezi kufanya jambo baya, nilimuokota kama mwanadamu mwenzangu sikujua kama muasi,” dereva alijitetea.
“Nyamaza mbwa wee!” alinyamazishwa na kofi zito la shavu.
“Pamoja na kunipiga lakini huko nyuma tumejulishwa waasi wanakuja.”
“Acha kututisha lazima upate hukumu ya kifo omba sala za mwisho kabla risasi haijafumua vichwa vyenu,” alisema kiongozi wao.
Dereva na msaidizi hakuwa na la kufanya, moyoni walijilaumu kwa wema utakaokuchukua uhai wao bila kosa lolote.
“Muteba na Kawelee malizeni kazi.”
Kiongozi alitoa amri ya dereva na msaidizi wake wauawe kwa risasi, waliwavua mashati yao na kuwafungwa usoni ili wasione wanavyouawa. Kisha kiongozi alitoa amri ili wapigwe risasi kwa kuwaeleza waweke silaha zao tayari kisha alihesabu.
“Moja…mbili….”
Kabla hajamalizia tatu mlio wa risasi ulisikika huku lori lililokuwa limebeba askari wa waasi likifunga breki mbele yao vilifanya askari wote waruke pembeni. Kwa mbali waliliona limesimama wakajua limeharibika kwa vile lilikuwa limesimama kwenye kona hawakuwaona haraka wanajeshi wa serikali. Majibishano ya risasi yalianza huku majeshi ya serikali yakijitahidi kuyadhibiti ya waasi. Milio ya risasi ilitawala eneo lile huku dereva na utingo wake wakiwa bado wamepiga magoti mikono yao juu wakiamini risasi zote zilikuwa zikiwakosa wao.
Vilio vya maumivu ya risasi vilifanya waamini kuna vita na kuwafanya wateremshe mikono na kujifungua mashati waliyofungwa.
Walikuta majibishano ya risasi katika ya majeshi ya serikali na waasi baada ya kuliona lori lao waliloelezwa limechukuliwa na waasi.
“Bosi tukimbie tutakufa,” msaidizi wa dereva alimshtua bosi wake.
Walitimua mbio mpaka ndani ya gari na kuliondoa kwa kasi. Nyuma walisikia risasi zikipiga kwa nyuma ya gari. Walikuwa waasi baada ya kuona gari walilokuwa wakilifuata ili kumuua Kamanda Janette na mama yake likiondoka huku wakiwa wamezuiwa na majeshi ya serikali.
Dereva baada ya kutoka eneo la vita salama alilikimbiza gari ili kuhakikisha anatoka salama baada ya kupona kifo. Aliendesha gari na kuweza kuingia salama Mji wa Bondo uliokuwa mpakani mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Kati.
Baada ya kusimamisha gari kwanza dereva alishusha pumzi nzito na kumshukuru Mungu kwa muujiza alioufanya juu yao kuwatoa katika kinywa cha mauti. Baada ya kufanikiwa kufika Bondo salama kazi ikawa kuwapeleka hospitali.
“Bosi tutafanyaje kuwapeleka hospitali na nguo za jeshi, lazima itatuletea matatizo.”
“Hapo ndipo kichwa kinaniua, tungejua tungewatupa porini ili kujiepusha na balaa hili, tukishikwa nao lazima tutafunguliwa mashtaka ya kuficha waasi na kufungwa kifungo kikubwa.”
“Lakini bosi kama wangekuwa waasi wasingefukuzwa na wale jamaa.”
“Hizi nguo alizovaa mmoja si unaona zina tofauti na jeshi la serikali.”
“Basi atakuwa amechoka na kuamua kutoroka.”
“Sasa tutafanyaje maana kila dakika moyo unanilipuka kila nikikumbuka malaika wa mauti aliyekuwa amesimama mbele yetu.”
“Kwa vile tumeamua kuwasaidia hatuwezi kuwapeleka na magwanda yao. Tukawanunulie magauni na sandozi tuwavisha na kuwapeleka hospitali binafsi kuepuka maswali,” msaidizi alitoa wazo.
“Kiwembe una mawazo ya maana sana.”
Dereva ambaye ndiye aliyekuwa mwenye biashara ile alimtuma msaidizi wake kufuata nguo duka la jirani. Baada ya kuletwa waliwavua magwanda na kuwavisha nguo za kawaida kisha waliwapeleka katika hospitali moja binafsi.
“Naomba uwahudumie kwa gharama yoyote wagonjwa wangu.”
“Hakuna tatizo Mutimwana wewe ni mtu mzito sana.”
“Nitashukuru.”
Baada ya Mutimwana kuwakabidhi wagonjwa na kulipa gharama za matibabu aliondoka na kumweleza daktari kuwa atarudi baadaye kuwajulia hali wagonjwa wake.
Huduma ilianza mara moja kwa kufanya vipimo vya haraka kwa Rosemary aliyekuwa bado amepoteza fahamu na kuonekana sumu imejaa kwenye damu. Walimchoma sindano ya kutoa sumu na kutundikiwa drip na kumwacha apumzike.
Kamanda Janette alipatiwa huduma kwenye jeraha la risasi na kuachwa naye apumzike kwa vile jeraha halikuwa na madhara makubwa.
***
Kamanda Janette alikuwa wa kwanza kuamka usingizini, alifumbua macho taratibu kuangalia yupo wapi. Alijikuta amelala kwenye kitanda, alipepesa macho taratibu kila kona na kugundua pale ni hospitali na kitanda cha pembeni alikuwa amelala mama yake huku mkononi akiwa na mpira wa drip iliyokuwa imeisha.
Hakutaka kuamka mara moja alitulia akiwaza pale ni wapi na wamefikaje. Alijinyanyua taratibu na kugundua kasoro kwenye mwili wake baada ya kusikia maumivu upande wa bega la kulia. Aliupeleka mkono taratibu na kulakiwa na bandeji kubwa. Alitabasamu baada ya kukumbuka ile ilikuwa risasi ambayo kama si umahiri wake wa kukwepa basi ingechukua uhai wake.
Kumbukumbu zake zilimuonyesha kuwa walikuwa porini ambako hapakuwa na kitu chochote cha kuwaponya hasa baada ya kushuhudia mama yake akiumwa na nyoka na kukosekana tiba yoyote, wakati huo naye alikuwa tayari ana jeraha la risasi lililosababisha apoteze damu na nguvu nyingi.
Ubora wa chumba cha hospitali ulionyesha ipo mjini lakini bado alibakia na swali nani aliyewapeleka pale na aliwaona wapi? Kingine kilichomuumiza kichwa kilikuwa vazi alilovaa, lilikuwa gauni la kawaida na si gwanda alilokuwa nayo. Alimuangalia mama yake naye alikuwa kwenye vazi la gauni.
Aliteremka kitandani na kwenda alipolala mama yake aliyekuwa bado amesinzia, alimbusu kwenye paji la uso na kusema kwa sauti ya chini.
“Mama nakupenda.”
Busu lile lilimfanya mama yake afumbue macho, kwanza alishangaa kujikuta katika mazingira yale.
“Vipi mama?” alimuuliza kwa sauti ya chini.
“Namshukuru Mungu kama mpaka sasa nipo hai nina imani nimepona, na hapa ni wapi?” mama yake alimuuliza huku akikaa kitako.
“Hata mimi mwenyewe sijui tupo wapi.”
“Na hizi nguo, tena zinaonekana mpya kwa harufu yake.”
“Atakayeingia atatupa jibu.”
Wakiwa katikati ya mazungumzo mlango uligongwa na kuwafanya wote washtuke na kunyamaza. Walitazamana, Janette kabla ya kujibu alinyata hadi mlangoni na kuchungulia nje.
“Mungu wangu,” alisema huku akishika kifua, kitu kilichomshtua mama yake.
“Kuna nini?” aliuliza macho yamemtoka pima. Alimwita mama yake kwa ishara ambaye alisogea mlangoni amsikilize mwanaye.
“Kuna nini?” alimuuliza kwa sauti ya chini.
“Wanajeshi wa serikali.”
“Wamejuaje tupo huku?”
“Hata najua yaani hilo swali wa kulijibu labda daktari.”
“Wafungulie.”
“Hapana si kirahisi kiasi hicho,” Janette hakuwa tayari kuwafungulia badala yake alifunga kwa komeo la ndani.
Mlango ulisukumwa kwa nje ili ufunguke lakini ulikuwa mgumu. Wanajeshi wa serikali wanagonga mlango wakati Janette amekataa kufungua.
Nini kitafuata kama wakiendelea kukaidi amri ya kufungua mlango. Ili kujua yote tukutane katika Championi Jumatatu.

Tags
Hadithi & Simulizi